SERIKALI imesema hairidhishwi na utoaji wa Fedha za gawio kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero (KSC) licha ya ukubwa wake na uzalishaji Mkubwa wa sukari kwa sasa.
Kauli hiyo imetolewa Jana na naibu waziri Wa Kilimo na Ushirika Omary Mgumba wakati alipotembelea na kujionea uzalishaji na uhifadhi wa sukari katika kiwanda hicho.
Mgumba alisema serikali haifurahishwi na utoaji Wa gawio hilo licha ya kumiliki hisa asilimia 25 za kiwanda na kuitaka menejimenti kutoa kwa wakati gawio hilo na ndipo serikali itaona njia gani za kuweza kukisaidia kiwanda hicho.
"Haiwezekani viwanda vidogo vya sukari vinatoa gawio kubwa na kwa wakati na nyinyi mna kiwanda kikubwa tu hapa lakini mmekuwa wagumu kutoa gawio kwa wakati, sasa ndugu zangu jirekebisheni huu uwekezaji tuliouwekeza huku tunataka tupate mafao makubwa zaidi,"alisisitiza Mgumba.
Alisema kwa sasa wameamua kuinua Kilimo na uzalishaji Wa miwa na njia ya kufanikiwa ni lazima uwepo ushirikiano baina ya viwanda,wakulima na serikali na hiyo ndio nguvu ya kiuchumi.
Ameipongeza KSC kwakuisikiliza serikali na kuweka bei nzuri ya tani ya miwa kwa wakulima Wa nje nakusema kuwa hayo ni Maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia upungufu Wasukari ya viwandani ambapo imepelekea kuingizwa kinyemela sukari tokanje,Mgumba alisema kama tunataka kutibu sukari ya magendo toka nje ni lazimatuwe na uzalishaji Wa kutosha Wa sukari ya viwandani toka ndani.
Alisema tunatakiwa kujenga uchumi wetu kwa uzalishaji zaidi nchini kwani inasaidia kupatikana kwaajira kwa wananchi wengi wazawa na pia kuuza ndani na nje ya nchi sukari yetu.
Awali mkurugenzi Mkuu Wa KSC Guy Williams alisema kwa sasa uzalishaji Wa sukari umeongezeka kwani hivi sasawamehifadhi tani 74,000 huku uwezo wao Wa kuhifadhi ni tani 60,000.
Alitaja sababu za kuongezekauzalishaji ni kutokana na kuchelewa kunyesha mvua na kusema kuwa Mpango waohivi sasa kupanua kiwanda na kuzalisha tani 265,000 toka uzalishaji tani130,000 kwa mwaka.
Aidha mkurugenzi huyo alisema pia wanampango wa kuongeza wakulima wa nje kutoka 8000 hadi kufikia wakulima16,000 na pia kwa sasa wanatanua soko lao ambapo hata mtu akihitaji tani moja anauziwa kiwandani.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa