Pichani juu: Katibu mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ally akizungumza na Wananchi
KATIBU Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi(Ccm) Taifa Dk Bashiru Ally amepiga marufuku mashindano yanayoandaliwa na viongozi Wa kuchaguliwa kuitwa majina yao na badala yake kutumia majina ya waasisi Wa taifa hili.
Akizungumza na wanaCcm katika mkutano wake uliofanyika Jana uwanja Wa Tangani mjini Ifakara,Dk Bashiru alisema haileti picha nzuri kwa kipindi hiki Mbunge ama Diwani kuandaa mashindamo mbalimbali, akitumia jina lake na hii itaonyesha ameanza kujinadi kabla ya muda.
"Mashindano yanaweza tumika vibaya hasa wakati huu kuelekea ktk udiwan, ubunge na urais kuwa ni sehemu ya kujinadi kabla ya muda,hivyo tutumie majina ya waasisi wetu ili kuondoa mgangano huo,"alisisitiza.
Bashiru ametoa kauli hiyo baada ya Mbunge Wa Viti maalum Mchungaji Dk Getrude Rwakatare kumueleza kuwa, toka ateuliwe na Rais Dk Magufuli amefanya mambo mengi, ikiwamo kuwaunganisha Vijana katika mashindano maalum aliyoyaandaa, yaliyokuwa yakijulikana kwa jina la Rwakatare Cup.
Aidha Amesema kuwa, licha ya mashindano hayo kumalizika, ila kwa sasa Mbunge huyo akitaka kuanzisha mashindano mengine, itabidi atumie jina la Kawawa na mashindano yatajulikana kwa Kawawa Cup badala ya Rwakatare Cup.
Amebainisha kuwa kwa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mwakani hapendi kuona mwanaCcm akimlalamikia mwanaCcm mwenzie eti amecheza rafu kwa kujinadi kabla ya muda kufika.
"Wapo wenye nia wanaweza ogopa kwa kuona baadhi wanafanya mambo kama hayo kwani uzani unaweza usiwe sawa kwa wananchi na wanaccm,"alisema.
Amewataka wana Kilombero waendelee kutembea kifua na kuchapa kazi kwani taifa linawatambua kwa uzalishaji mzuri Wa zao la mpunga na kudai kwa sasa nchi ina chakula kingi cha kutosha.
Pia amewataka wananchi kuacha kugombana kwa sababu ya vyama vya siasa na kusema kuwa vyama visiwe chanzo cha kututenganisha bali vitumike kutuunganisha.
Kuhusu uandikishaji Wa wanachama wapya,Dk Bashiru aliwataka viongozi kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya kuendelea zoezi la uandikishaji na waache tabia ya kudai kwanza Fedha ya kadi na kusema wawasajili kwanza na Fedha kuchukua baadae.
Awali Mbunge Wa Viti maalum Mchungaji Dk Gertrude Rwakatare amesema toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali.
Dk Rwakatare amesema nae toka ateuliwe amezunguka majimbo yote mawili, na kutoa misaada mbalimbali ndani ya chama na serikalini ikiwemo kutoa mikopo kwa akina mama, kugawa kadi za Ccm kwa wanachama wapya zaidi ya 70,000 na kutoa baiskeli 300 kwa makatibu Wa Kata na matawi Wa Ccm.
Nae Mwenyekiti Wa Ccm Wilaya ya Kilombero Clarence Mgomba alisema kuwa, Wilaya ipo vizuri kwa sasa kwani ushirikiano baina ya chama na watendaji Wa halmashauri zote ni Mkubwa.
Amemshukuru Rais kwa kuwapatia halmashauri Mbili za Mlimba na Ifakara na kumuahidi kuwa mwaka 2020, hawatakuwa na Mbunge Wa kuteuliwa bali watakuwa na wabunge Wa kuchaguliwa katika majimbo yote mawili.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa