Halmashauri ya wilaya ya kilombero imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa viongozi wa kijiji cha ikwambi kata ya mofu tarehe 24/2/2018, kata hiyo imepokea msaada wa vifaa hivyo vya zahanati ya kijiji hicho baada ya upepo mkali kuezua mabati na kuharibu jengo hilo, hali iliyopelekea wananchi kukosa huduma hiyo muhimu sana kwao.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, mheshimiwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilombero ndugu Daudi Ligazio alisema kuwa serikali imeamua kuleta vifaa hivyo kwa haraka sana kutokana na ukweli kwamba inawathamini wananchi wa maeneo tofautitofauti na kijiji cha Ikwambi kikiwa ni mojawapo.
Aliendelea kusema kuwa anawaomba wanakijiji hao wathamini sana miradi inayoletwa na serikali kwani ni kwaajili yao wenyewe na kushauri kuwa umefika wakati sasa wapunguze matumizi ya dawa za kienyeji na kuanza kuitumia zahanati hiyo kwani ndo msaada na kama kuna hujuma zozote ambazo zahanati hiyo inafanyiwa basi wahakikishe wanaachana na hujuma hizo kwani inaweza kuwaletea matatizo makubwa sana.
Akipokea msaada huo diwani wa kata ya mofu alisema kuwa anashukuru sana kwa msaada huo kwani ujio wa vifaa hivyo umekuja kutatua matatizo wa vijiji vitatu ambavyo ni Klenga, Mofu na Ikwambi, kwani matumizi ya kadi ya CHF ambayo ndio nafuu pekee kwa wakazi hao, inapatikana kwenye zahanati hiyo pekee.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa