Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili. Dunstan Kyobya @kyobyad @dc.kilombero ameongoza kikao Cha Kamati ya lishe Cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi Cha Julai- Desemba 2023 na kuelekeza Watendaji kusimamia uchangiaji wa chakula shuleni na kwa kusimamia ulaji wa makundi matano ya vyakula ili kuimarisha lishe mashuleni. Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero amewaelekeza Wakuu wa Divisheni za Elimu ya Awali na Msingi pamoja na Sekondari kusimamia uundwaji wa klabu za lishe, mazingira, klabu za kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, Klabu za kupinga ukatili na Kijinsia na watoto. Vilevile, Mkuu wa Wilaya ameelekeza Halmashauri kuongea afua za lishe kwa kutafuta wataalamu wa usindikija vyakula na kutembelea wenye viwanda vya vyakula ili kutoa elimu ya kuongeza virutubisho katika uzalishaji wa vyakula.
Mkuu wa Wilaya amezungumzia hayo leo alipofanya kikao cha kufanya Tathimini wa utekelezaji wa afua za Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kwenye ukumbi wa Hospital ya Wilaya. @wizara_afyatz
https://www.instagram.com/p/C3AmjegIesc/?igsh=YjVzaWxlbnZlcTht
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa