Pichani juu: Mkuu wa kitengo cha Mifugo na uvuvi Kilombero (mwenye kofia ya rangi ya chungwa) Dokta Annete Kitambi, akipiga makofi huku akimsikiliza moja ya viongozi walipotembelea kata ya Mchombe.
Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kupitia afisa mifugo na uvuvi, Dr. Annete Kitambi, mwishoni mwa wiki iliyopita, imefanikiwa kuhamasihsa uchanjaji wa kichaa cha mbwa kwa mbwa wote waliopo katika kata zaidi ya nne ambazo ni Igima, Mchombe, Mbingu na Mgeta, na wamekwishafanikiwa kuwachanja mbwa hao kwa gharama za wamiliki wa mbwa hao.
Hayo yamesemwa na Dokta Kitambi alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, pale mwandishi alipotaka kujua kuwa kutokana na wimbi kubwa sana la kung’atwa kwa watu na mbwa hao, kama halmashauri wamechukua hatua gani.
Akitoa tathmini ya zoezi la uchanjaji wa mbwa hao katika maeneo hayo, Dokta Kitambi alisema kuwa, tayari mbwa zaidi ya sitini tangu jumamosi hii, wamekwishachanjwa na kupumzishwa, huku akisema kuwa kwa kushirikiana na mganga mkuu wa Halmashauri ya Kilombero, Dokta Samwel Lema, tayari waathirika wote waliong’atwa na mbwa hao wamekwishapatiwa chanjo, huku chanjo nyingine za binadamu (Vial) zaidi ya tisa zikiwa zimepelekwa huko kwa usalama zaidi wa wananchi ambao watakumbwa na mkasa wa kung’atwa, ingawa bado chanjo nyingine zaidi ya thelathini zinahitajika.
Nae mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Dokta Samweli Lema, amesema kuwa, tayari wamekwishaagiza chanjo za binaadamu zaidi ya 200 kutoka Bohari kuu ya madawa (MSD), kwaajili ya tahadhali kwa wananchi wote watakaopatwa na mkasa huo wa kung’atwa na mbwa, ambapo chanjo hizo amesema kuwa zitatolewa bure kabisa, kwa wananchi wote wa wilaya ya Kilombero.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa