Pichani juu: Miongoni mwa mazao ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero inatarajia kuyaonyesha kwenye kipindi cha Nanenane.
halmashauri ya wilaya ya Kilombero imejizatiti vya kutosha kuingia kwenye maonesho ya kilimo Nanenane yatakayofanyika kimkoa katika mkoa wa Morogoro kwenye eneo la maonyesho hayo yanayopatikana eneo la Nanenane, kwaajili ya kuonyesha mazao mbalimbali yanayopatikana wilaya ya kilombero.
Akitoa ufafanuzi juu ya hali ya maendeleo ya vipando hivyo, Afisa Kilimo wa Hlamashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Mohammed Ramadhani alisema kuwa , kwasasa hali imezidi kuimarika na mazao yanakwenda vizuri na yapo katika hali ya ubora kabisa kwaajili ya kuonyeshwa kwa wananchi ili waweze kujifunza njia bora na sahihi kwaajili ya kulima na kupata mazao bora.
Aidha bwana Ramadhani aliongeza kuwa kulikuwa na tatizo kubwa sana la upatikanaji wa maji katika maeneo hayo, ambapo tayari halmashauri imekwishachukua hatua madhubuti kabisa, kuhakikisha kuwa hali inakwenda vizuri na maji yamepatikana mengi, hivyo kufanya vipando kuonekana ni vyenye kunawiri mno.
katika hatua nyingine bwana Ramadhani, amechukua fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote kwenye maonyesho hayo ya Nanenane, ili kuweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakaazi wa Kilombero kwaajili ya kupata mafunzo Anuai.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa