Kampeni shirikishi ya kitaifa ya utoaji wa chanjo iliyofanyika kilombero kuanzia Tarehe 17 hadi 21 mwezi wa kumi imefanikiwa kwa asilimia kubwa baada ya chanjo hiyo kufanyika kwa asilimia zaidi ya matarajio
akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, mratibu wa masuala ya chanjo Bi Niindaeli Malugu amesema kuwa mpaka zoezi hilo linakamilika tayari walikwishachanja kwa 105% sawa na watoto 46720 ambapo waliowekwa kwenye mpango mara ya kwanza walikuwa watoto 44500 kwa chanjo ya Surua Rubela na 98% ya watoto 25747 ambao ni 25359 kwa chanjo ya polio ya sindano.
Aidha bi Malugu aliwashukuru kada tofauti wakiwamo viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, waandishi wa Habari pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha uhamasishaji na kufikia zaidi ya lengo lililowekwa.
Akiongezea kwenye taarifa yake mratibu huyo wa chanjo Kilombero amesema kuwa kutokana kujitokeza watoto wengi iliwalazimu kuongeza watoa huduma (TIMU) 21 sawa na wafanyakazi 105 kuongezea timu waliyopewa na wizara ya Afya ambayo ni 42 sawa na watendaji 210 na kufanya timu zilizohudumia kufikia62 sawa na wafanyakazi 315 ambao walijitokeza kusaidia umaliziaji wa wa chanjo hiyo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa