Pichani juu baadhi ya wadau wakimsikiliza mratibu wa mradi huu wa Lishe Edelevu Ndg Revocatus Kashaga
Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndg Ismail Mlawa amesema kuwa kuongeza virutubishi kwenye chakula kuna faida kubwa sana, hasa ukizingatia kuwa uandaaji wa vyakula hivyo huondoa virutubishi vyote vya vyakula hivyo, na hivyo kuviacha vyakula hivyo kuwa kama makapi ambayo hayana faida yoyote ile Zaidi ya kujaza tumbo tu wa walaji.
Ndg Mlawa ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika mngeta ambacho kiliwashirikisha wadau mbalimbali wa lishe katika wilaya ya Kilombero, katika kujadili kuhusu masuala ya lishe katika wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine, Mratibu wa mradi huo ndugu Revocatus Kashaga amesema kuwa wamejitahidi kwa kiasi kikubwa mno kushawishi shule mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaongeza virutubishi hivyo kwenye chakula na tayari wamekwishaanza na shule kadhaa kwani lengo lao ni kulenga Watoto walioko mashuleni hususan Watoto wa shule za ‘primary’.
Awali akitoa taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Mlimba, Afisa lishe wilaya ya Mlimba ndg Goodluck Simon amesema kuwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba kuna Watoto walio chini ya miaka 2 wapo Zaidi ya 15000 na wale walio chini ya miaka mitano ni 39,000 na kwa takwimu za mwezi oktoba mpaka disemba inaonesha kuwa kuna Watoto 13 walioripotiwa kuwa na utapia mlo mkali san ana tayari wamekwishapata matibabu kutoka kwenye vituo vya Afya vya Mlimba na Mgeta na mpaka sasa wanaendelea vizuri.
Nae mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Injinia Stephano Kaliwa amesema kuwa kwa sasa ukiangalia kwenye graph ya lishe kimkoa tupo katika nafasi ambayo sio nzuri hii inatokana na ukweli kwamba mwanzoni hatukuwa na wodi za Watoto wanaoumwa utapiamlo mkali hivyo kutulazimu kuwapeleka Watoto wote katika Hospitali ya Mtakatifu Francis iliyopo Ifakara kitendo ambacho kilikuwa kikiwapa maksi Ifakara hivyo kwa sasa hawataweza tena kurudi katika nafasi hizo mbaya kwani tayari wamekwishatenga wodi mbili ambapo moja ipo katika kituo cha Afya mlimba na nyingine ipo Mngeta.
Kikao hicho kimeandaliwa na wadau wa masuala ya Lishe ambao ni USAID LISHE ENDELEVU, na kinahusisha baadhi ya wakuu wa idara ambao huwa ni chanzo cha masuala ya lishe na wadau wote ambao ni Asasi zisizo za kiserikali ambazo zinahusiana na masuala ya lishe.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa