MKUU Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema kuwa baada ya Machi 31 mwaka huu Mifugo iliyosajiliwa NA kuwekwa alama ndiyo itajayotambuliwa wilayani humo na isiyokuwa NA alama itabidi iondolewe lasivyo itataifishwa.
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuzungumza na viongozi na wafugaji wa vijiji vya Bwawani,Nyamwezi na Kiberege katika kata ya Kiberege wilayani hapa.
Ihunyo alisema kwa sasa katika maeneo mbalimbali wilayani humo kuna makundi makubwa ya mifugo yanaingia kinyemela huku baadhi ya wafugaji wakificha Mifugo yao NA kukataa kuwekwa alama NA kusema kuwa serikali yake haitokubali Wilaya hiyo kuwa dampo la Mifugo kwa sasa.
Alisema hairuhusiwi kwa Mifugo kuingia katika Wilaya hiyo kwa sasa labda kwa mamlaka ya Afisa Mifugo Wilaya ambaye ndie mwenye mamlaka ya kutoa kibali NA kutoa rai kwa viongozi wote kuanzia ngazi za vitongoji hadi kata kutoa taarifa punde wanapoona makundi ya Mifugo yakiingia maeneo yao.
Aidha Mkuu huyo Wa Wilaya amewaagiza diwani na Mtendaji kata Wa Kiberege kwa kushirikiana na maafisa Ardhi kukagua kisha kutoa ekari 1000 za Ardhi ambazo zilitolewa enzi ya kijiji kimoja cha Kiberege kwa wafugaji ambapo toka mwaka huo hadi Leo hazijatolewa.
Kuhusu kutatua migogoro ya wakulima NA wafugaji,Ihunyo aliziagiza serikali za vijiji kubainisha maeneo yao NA kutenga maeneo ya wafugaji kama yatakuwepo NA pia wakitengeneza njia kwa ajili ya kunyweshea Mifugo sambamba NA kutengeneza malambo.
Amebainisha kuwa viongozi wengi Wa vijiji wamekuwa ndio vyanzo vya migogoro katika maeneo yao hivyo kuwataka wabadilike lasivyo atakaebainika atamshughulikia.
Awali jamii ya wafugaji wanaoishi katika kata hiyo walilalamikia viongozi Wa vijiji kutowapatia eneo la ekari 4623 walizopewa NA kijiji kimoja enzi hizo kinaitwa Kiberege kabla ya sasa kuwa NA vijiji vitatu vya Kiberege,Nyamwezi na Bwawani.
Mmoja Wa wafugaji hao Kazingoma Kushonga alisema eneo la wafugaji lilitengwa toka mwaka 2003 NA kukamilika mwaka 2004 katika kukamilisha Mpango Wa matumizi bora ya Ardhi ambapo walichangia shilingi milioni moja ili kukamilisha Mpango huo.
Kushonga alisema baada ys zoezi kukamilika walikuwa wakisubiri kukabidhiwa eneo lao lakini wamezungushwa toka kipindi hicho hadi Leo licha ya uongozi Wa mkoa kuagiza wafugaji hao kupewa eneo lao.
Naye Bony Nangeleki alisema wakati wakiendelea kusubiri eneo lao wakashangaa katika mkutano Wa January 13 mwaka huu vijiji vyote vitatu kudai kuwa hawana eneo la wafugaji wakati wao wanaelewa eneo lao lipo katika vijiji vipya vya Nyamwezi na Bwawani ambapo hivi sasa maeneo hayo yamelimwa NA wakulima.
Ndipo diwani Wa kata ya Kiberege Shabani Mlango alipoinuka NA kusema kuwa kweli enzi ya kijiji kimoja wafugaji waliomba eneo la ukubwa huo lakini wananchi waligoma kutoa ekari hizo 4623 na kubariki ekari 1000 tu tokana NA uchache Wa wafugaji kuwa sita tu.
Mlango alisema lakini baadae ekari hizo 1000 zikaleta mgogoro baada ya mfugaji mmoja kudai ekari zake 460 alizonunua kijijini na alishinda kesi hivyo wao kuamua kugawa ekari 460 katika ekari 1000 walizotenga NA baada ya vijiji kugawanyika zikaonekana ekari hizo 1000 zipo katika kijiji cha Bwawani.
Baada ya Maelezo hayo Mkuu Wa Wilaya aliagiza uongozi Wa kata NA wataalamu Wa Ardhi kubainisha hizo ekari 1000 NA kisha kugawa ekari 460 kwa mfugaji pale watakapojirisha hukumu iliyotolewa NA ekari nyingine 540 wapewe wafugaji ili kumaliza mgogoro huo.
Hatahivyo wafugaji hao bado walipingana NA maagizo ya Mkuu Wa Wilaya kwa kusema kuwa kwa kufuata haki basi wanatakiwa kupewa ekari 1000 kama walivyokubaliwa NA mkutano Wa kijiji NA ekari 460 za mfugaji aliyeshinda kesi kijiji kinatakiwa kimpatie nje ya eneo hilo kwani alizinunua kihalali NA sio maombi ya wafugaji.
Mwisho....
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa