Pichani juu: mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mh. Innocent Mwangasa akiongea na baadhi ya washiriki (Hawapo pichani) kuhusiana na siku ya mtoto wa Afrika
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hapo jana yamefana kwa kiasi kikubwasana katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba ambapo Watoto mbalimbaliwalishiriki katika kuonesha vipaji mbalimbali na kufundishwa mambo mbalimbaliyanayohusiana na haki zao, katika upande mwingine wazazi wamekumbushwa namnabora ya kuwalinda Watoto wao ili wasipate matatizo yoyote katika Maisha yao nakufanikisha ndoto zao bila kikwazo chochote kile.
Hayo yamesemwa na kaimu Mkurugenzi Dr. Christina Guvetti alipokuwa akitoasalamu za mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Dr. Guveti ameongeza kuwa Halmashauri, CAMFED Pamoja na Plan Internationawaliandaa mikakati mbalimbali juu ya ulinzi wa mtoto aliyepo katika Halmashauriya wilaya ya Mlimba, mipango Madhubuti pia imefanywa kwenye suala la elimu nahilo limefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa sana mfano kwa mwaka 2019 kiwangocha ufaulu kilikuwa ni 86.6% wakati 2020 kiwango kiliongezeka na kufikia 95.3%.
Katika hatua nyingine Dr. Guveti alisema kuwa wazazi wasikubali Watoto waokuishia kidato cha nne pekee, kwani kwa sasa Halmashauri imefanya jitihada zakusajili shule mbili ya Nakaguru na Kiburubutu kufundisha Watoto wa kidato chatano na sita, hivyo hii ni fursa kwa Watoto wa Halmashauri hii, shule hiiisiachwe kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Halmashauri kuja kujaza shule hizi,wanafunzi wa hapa wanatakiwa kujitahidi kwa kila hali kufanya vizuri ili wawezekupata nafasi hapahapa nyumbani.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba ambae pia ni Diwani wakata hiyo ya Igima Mh. Innocent Mwangasa amesema kuwa anaungana na Mkurugenzikwa kuwaasa wazazi waanze wao kuwalinda watoto wao kisha wengine wafuate, nawale ambao wamezoea kuwanyanyasa Watoto wakae chonjo kwani dawa yao inachemka.
Akiendelea kusisitiza, Mh. Mwangasa amesema kuwa walimu wakuu wote katikaHalmashauri hiyo ambao wana tabia ya kushirikiana na wazazi na wahalifu kufichauovu wa kuwapa ujauzito Watoto, walimu hao hawana nafasi kwenye shule zilizokokwenye Halmashauri yake na ataanza kuwachukulia hatua kali za kinidhamu ikiwamokufukuzwa kazi kwani wao ndio chanzo cha Watoto kufanyiwa ukatili wa kinyamakatika jamii zao.
Siku ya mtoto wa Afrika, huadhimishwa kila mwaka barani Afrika kupingamauaji na ukatili waliofanyiwa Watoto wa huko Afrika kusini na makaburu, mauajihayo yalifanyika katika kitongoji cha SOWETO mwaka 1976 wakati Watoto haowalipokuwa wakiandamana kudai Haki zao za msingi.
Habari Picha.
Pichani chini mwenyekiti wa baraza la watoto la wilaya ya Mlimba akiongea jambo na watoto wenzake pamoja na wageni waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo
pichani mgeni Rasmi ambae ni kaimu Mkurugenzi Dr. Christine Guveti akiwa Mwenyekiti na Katibu wa baraza la vijana katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mapema janaWageni mbalimbali waliohudhuria katika shughuli hii ya siku ya Mtoto wa Afrika
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa