Pichani juu:Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg Ismail Mlawa (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye kikao cha kwanza cha baraza la madiwani.
MADIWANI katika halmashuri ya wilaya ya Mlimba mkoani Morogoro wametakiwa kuchukua mawazo ya wananchi wanaowaongoza na kuyaleta katika vikao vya madiwani na sio kuleta mawazo yao binafsi.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na mkuu wa mkoa wa Morogoro Olata Ole Sanare wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika tarafa ya Mngeta wilayani hapa.
Akimwakilisha mkuu huyo wa mkoa,Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ismail Mlawa alisema kama madiwani hao wapya wakichukua mawazo yao binafsi na kuleta katika mabaraza watakuwa hawawatendei haki wananchi wanaowaongoza kwani mawazo ama changamoto za wananchi zinaanzia katika vikao vya chini kasha kuletwa katika baraza la madiwani.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kama diwani atakuwa analeta mawazo yake yeye katika baraza basi diwani huyo atakuwa hafanyi mikutano katika kata yake ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na hivyo atakuwa anavunja miiko ya Chama chake kilichomuweka madarakani.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa serikali haitarajii kuona kunakuwepo mivutano baina ya madiwani na watendaji ukizingatia kuwa madiwani wote katika halmashauri hiyo ni wa kutoka Chama cha Mapinduzi(Ccm) hivyo kutegemea uwepo ushirikiano utakosaidia kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Sanare amewataka madiwani hao wasimamie ukusanyaji wa mapato kwa kufuata sheria na waweke ubunifu katika kuanzisha vyanzo vipya vya mapato huku pia akiwakumbusha kuwa ni wajibu kutenga asilimia 10 kwa ajili ya mikopo kwa vijana,wanawake na makundi maalum.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Innocent Mwangasa aliwashukuru madiwani wenzie kwa kumpatia yeye na makamu wake ushindi wa asilimia 100 na kudai kuwa ana deni kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mlimba na kusema kuwa shauku yake ni kuona Mlimba inapiga hatua katika maendeleo.
Mwangasa alisema licha ya kujiwekea mipango mingi mmojawapo ni kushirikiana na mkurugenzi mtendaji,mbunge na watendaji wengine na pia akihakikisha kila diwani katika kata yake anatimiza wajibu wake katika kusimamia kata na kutatua kero za wananchi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa