HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilombero inakadiriakukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3,942,213,600.00 kutoka vyanzo vyake vya ndanikwa mwaka Wa Fedha 2018/2019.
Akizungumza katika kikao maalum cha kupitishabajeti ya halmashauri hiyo,mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri hiyo Dennis Londoalisema makadirio hayo yameongezeka kwa shilingi milioni 338,003,600.00 ikiwani Sawa na ongezeko LA asilimia 9 kulinganishwa na makadirio ya shilingibilioni 3,604,210,000.00 ya mwaka Wa Fedha uliopita 2017/2018.
Sambamba na hilo halmashauri hiyo kwa mwaka WaFedha 2018/2019 inakadiria kupata jumla ya shilingi bilioni 47,056,355,278.00kutoka vyanzo mbalimbali.
Londo alisema uandaaji Wa bajeti hiyo unazingatiamaeneo mahusudi na ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango mkakati Wahalmashauri Wa mwaka 2016/2017-2020/2021.
Ameyataja maeneo hayo kisekta kuwa no kilimo naMifugo,elimu ya msingi na sekondari,Afya,Maji,miundombinu,utawala,Fedha naMipango,uvuvi na Ardhi,maliasili na Misitu.
Akielezea mwaka unaomalizika Wa 2017/2018,Londoalisema halmashauri iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 40.5 kutoka vyanzombalimbali kwa ajili ya utekelezaji Wa shughuli mbalimbali na hadi kufikiaDisemba 2017 halmashauri ilishakusanya jumla ya shilingi 17.207,371,624.60 Sawana asilimia 42.49 ya makisio ya mwaka.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa hadi kufikuanusu mwaka 2017/2018 halmashauri kupitia mapato yake ya ndani na Fedhailiyopokelewa kutoka serikali kuu imefanikiwa kufikia mafanikio mbalimbaliyakiwemo kukamilika kwa mradi Wa Maji kijiji cha Msolwa Ujamaa na Nyange namradi Wa uchimbaji visima 50 vya Maji kwa kushirikiana na shirika LA HVC nahalmashauri.
Pia utekelezaji Wa mradi Wa Waridi kuimarishwa nakukarabati miundombinu ya Maji katika Kata za Kiberege,mang'ula naKidatu,ukamikishaji Wa vyumba vya madarasa 89 matundu ya vyoo na Nyumba zawalimu katika shule za msingi,vijiji 13 vimefanikiwa Mpango Wa matumuzi bora yaArdhi na hati 18953 za kimila zimeandaliwa na vipande vya Ardhi 22040vilipimwa.
Hata hivyo mkurugenzi huyo ametaja changamotombalimbali zilizokawia kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo kuchelewakupatikana kwa Fedha za miradi hasa za ruzuku ya Maendeleo kwa serikali zamitaa,itikadi za vyama vya kisiasa kuingizwa kwenye miradi ya Maendeleo nawakandarasi wengi kukosa uwezo Wa kifedha kukamilisha miradi kwa wakati.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa