Pichani juu: Mh Samia Suluhu Hassan akiapa mara baada ya matakwa ya kikatiba kumtaka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, mapema leo ameapishwa na kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa mama Samia amesema kuwa tofauti na siku nyingine zote ambazo huapa kwa nderemo na vifijo, leo ni siku ngumu sana kwake ambapo anaapa kwa majonzi makubwa sana, kwani Tanzania tumempoteza kiongozi shupavu na muadilifu mno.
Baada ya Kiapo hicho, mama Suluhu alikagua gwaride baada ya kupigiwa mizinga kadhaa ya heshima na kisha akapata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kuwasihi wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu huku akitoa ratiba ya mazishi ya kiongozi wetu huyu na kusema kuwa sasa siku ya maombolezo zitakuwa 21 na siku ya Jumatatu ambapo mwili utapelekwa Dodoma na siku ya mazishi ambayo ni Alhamisi zitakuwa ni siku za mapumziko.
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan, analazimika moja kwa moja kushika nafasi ya urais akipokea kijiti kutoka kwa Hayati Dokta John Pombe magufuli na atalazimika kuongoza kwa kipindi chote cha miaka minne iliyobaki na kwakuwa anakuwa ni mwingine sasa ni Rasmi kuwa kipindi hiki kitaitwa ni cha awamu ya Sita.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa