Afisa elimu wa Mkoa wa Morogoro Injinia mwalimu Joyce Balabuga amesikitishwa na kupatikana kwa vijana mamluki ambao hawakustahili kujiunga na michezo hiyo ya UMINTASHUNTA ikiwa ni kati ya watoto 616 ambao waliwasili kambini kwa ajili ya michezo hiyo mamluki ni vijana 34 ambao wametokea katika shule za sekondari na vyuo huku wanaostahili ni vijana kutoka katika shule za msingi.
Akizungumza katika zoezi la ufungaji wa michezo hiyo ya UMINTASHUNTA katika vuwanja vya shule ya sekondari ya wanawake Ifakara Balabuga amesema kuwa kitendo hicho kimemsikitisha sana kwani michezo ni maadili lakini bado wamepatikana watu waliovunja maadili hivyo kuomba vitendo vya namna hyo visijirudie tena kwa awamu zijazo.
Kwa upande wake Monica Saile Andrew ambaye ni kaimu mkurugenzi katika Halmashauri ya mji wa Ifakara amempongeza Injinia Joyce Balabuga kwa kuwabaini mamluki walioingia katika michezo hiyo huku akitoa mapendekezo yake kwa Halmashauri kutenga bajeti ya michezo ili kuwawezesha maafisa michezo na walimu kwa ujumla kutumia vema taaluma zao kwa ufasaha.
Lakini pia Andrew ametoa rai kwa walimu nwa michezo kuwafundisha watoto michezo ili kujenga vipaji na sio kuwachukua mamluki ambao wanakuja kwa lengo la kuwazibia nafasi zao kwa wale wenzao wanaostahili.
Aidha afsa michezo wa Mkoa wa Morogoro Grace Njau, ameeleza moja ya changamoto iliyoikabili michezo hiyo ua UMINTASHUNTA kwa kipindi hiki ni kwa baadhi ya walimu na makocha kuwaingiza watu wasiostahili kushiriki katika michezo hiyo(mamluki)
Ikumbukwe kuwa vijana hao waliwasili katika kambi hiyo mnamo tyarehe 14/6/2019, ambapo wakiwa jumla ya wanafunzi 616 wakiambatana na walimu 63 pamoja na madaktari 8, ambapo hali ya kambi ilikuwa sala huku lengo kuu la mashindano hayo ni kupata timu ambayo itawakilisha Mkoa wa Morogoro katika mashin dano ya kitaifa yatakayofanyika Mtwara kuanzia tarehe 23/6/2019 hadi tarehe 4/7/2019, pia kuinua vipaji vilivyopo katika ngazi ya wilaya, mkoa hadi kufikiakatika ngazi ya kitaifa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa