Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Chifu jAmes Ihunyo.
SERIKALI wilayani Kilombero imepiga marufuku kwa wenyeviti ama watendaji Wa ngazi za vijiji na kata kutoa vibali vya uhamishaji Wa mifugo na zoezi hilo sasa litasinamiwa na Afisa Mifugo Wa halmashauri.
Akizungumza na wananchi Wa Kata ya Mofu,Mkuu Wa Wilaya hiyo James Ihunyo amesema kumekuwa na tatizo la uingizwaji kinyemela Wa Mifugo katika kata hiyo na maeneo mengi wilayani na hiyo usababishwa na baadhi ya wenyeviti ama watendaji kuruhusu Mifugo kuingia ama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ihunyo amesema tatizo la uingiaji Wa Mifugo wilayani humo uchangiwa na viongozi ambao wapo tayari kupokea rushwa ili baadae kuleta migogoro ya wakulina na Wafugaji.
Amesema malalamiko mengi ya wananchi katika kata hiyo kuhusu migogoro ya wakulina na Wafugaji ni kuwa suala hilo uchangiwa na viongozi wao kwani wao ujali zaidi rushwa bila kujua athari za huko mbele.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuanzia sasa kibali cha kutoa Mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo jingine litafanywa na Afisa Mifugo kwa niaba yake na Mtendaji yeyote atakaejihusisha atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na hata kufukuzwa kazi.
Aidha Mkuu huyo Wa Wilaya amemuagiza mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephani Kaliwa kupeleka wataalamu ili kuhakiki usajili Wa Mifugo uliofanywa siku za nyuma na mfugaji yeyote aliyeongeza Mifugo itabidi Mifugo hiyo iondolewe haraka.
Katika hatua nyingine mkuu huyo Wa Wilaya amemtaka Meneja Wa pori tengefu Kilombero kupitia Mamlaka ya Usimanuzi Wanyamapori Nchini(TAWA) kuweka kambi katika eneo la Mofu tokana na eneo hilo kukithiri kwa Mifugo ibayoingia kwa wingi kutoka Wilaya Jirani za Ulanga na Malinyi.
Ihunyo amesema kwa sasa makundi makubwa ya Mifugo yapo katika eneo la hifadhi za pori tengefu na Tawa wakiweka kambi katika eneo hilo litasaidia kuzuia Mifugo mingi kuingia katika Kata hiyo sambamba na kata za Mngeta,Chita na Mlimba.
Awali mkurugenzi Mtendaji Wa halmashsuri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa alizitaja Jamii za wakulima na Wafugaji kuwa upendo na kuondokana na chuki kwani shughuli wanazofanya zinategemeana na wakizitumia vizuri changamoto zilizopo zaweza kuwa fursa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa