Pichani juu:Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Clifford Tandari akifungua rasmi michezo ya UMISETA.
Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Ndugu Clifford Tandari, mapema leo amezindua michezo kwa watoto wa shule za sekondari (UMISETA), katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ifakara (IFAKARA GIRLS).
Katika uzinduzi huo, Ndugu Tandari amesema kuwa, katika michezo kitu kinachotakiwa ni kucheza kwa kusaidiana na kuepuka kuumizana (Fair), ili kuweza kuimarisha michezo katika shule zetu.
Aidha Ndugu Tandari, amethibitisha kuwa, michezo huimarisha Afya ya ubongo, pamoja na kukuza uelewa wa kutosha kwenye michezo, hivyo amewaasa walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia michezo ipasavyo ili kuweza kuweka mambo sawa kwenye sekta hiyo.
Katika upande mwingine Afisa vijana na michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, ndugu Nicolaus Makata amesema kuwa, wamepokea kwa mikono miwili maagizo ya Katibu tawala huyo na wakiwa kama wasimamizi wa michezo hiyo, watahakikisha michezo hiyo inakwisha salama, na wanatimiza azma yao ya kuchagua baadhi ya wanafunzi watakaofanya vema kwenye michezo hiyo, kwaajili ya kuwakilisha mkoa kwenye michezo inayofuata.
Awali Ndugu Makata amesema kuwa, michezo hiyo imekuwa ikifanyika katika shule hiyo mfululizo kutokana na ukweli kuwa, shule hiyo ina mazingira mazuri sana ya Watoto kuweza kuishi, lakini pia imekusanya viwanja vya michezo yote ambayo michezo yake inashindaniwa, ikiwamo Mpira wa miguu na wa mikono, Mpira wa Basket, Mpira wa Net na michezo mingine yote.
Michezo hiyo ambayo iliwakutanisha wanafunzi wa wilaya mbalimbali mjini Morogoro, inategemewa kufungwa siku ya jumatatu, mara baada ya mechi zote kumalizika na wanafunzi wote kuweza kurudi mahali walipotokea.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa