Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa mapema leo amekutana na wasimamizi wa vituo vya Afya na Zahanati mbalimbali katika kikao kilichofanyika ofisini kwake
katika mazungumzo nao Mhandisi Kaliwa amewataka wasimamizi hao kufuata utaratibu unaotakiwa katika matumizi ya pesa ili kuhakikisha wanatumia pesa za makusanyo kwenye zahanati na vituo vya Afya wanavyovisimamia inavyopaswa ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza .
Akizungumza na wasimamizi hao wa vituo vyote katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mapema leo asubuhi, Mhandisi Kaliwa amesema, wasimamizi wote wa zahanati na vituo vya Afya wilayani hapa wanatakiwa kuepukana na matumizi ya pesa (Mbichi) ambazo hazikufuata utaratibu unaotakiwa wa matumizi yake.
Kwa upande mwingine Mhandisi Kaliwa amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanashirikiana na kamati inayohusika na dawa kuhakikisha kuwa wanahesabu kila dawa mpya zinazoingia katika vituo vyao vya kazi ili kuepuka sintofahamu ya kupotea kwa dawa mara kwa mara kitendo ambacho kinaweza kuwatia matatani wasimamizi hao.
Aidha amewaambia kuanzia tarehe 01/11/2020 wataletewa utaratibu mpya wa tozo mbalimbali zitakazotumika kwenye vituo vya Afya na zahanati zote na vituo vya afya kwani hadi sasa maandiko yamekwisha andaliwa na watayapata hivi karibuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.
Mwisho amewaomba kuwa wanyenyekevu katika utendaji wa kazi wao kwa kuepukana na lugha chafu wawapo kazini na kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi ili kusaidia jamii kufikia malengo yanayohitajika, kwani tayari amekwishapata malalamiko kadhaa toka kwa wananchi hivyo amewaonya kuwa makini ili kuepusha matatizo ya hapa na pale ya wananchi wao.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa