Pichani juu ni Katbu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo Katikati mwenye suti nyeusi akizindua msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2020/2021 katika skimu ya Njage wilayani mlimba tarehe 26/11/2020
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Mhandisi
Emmanuel Kalobelo amezitaka Halmashauri zote mkoani humo kuendelea kuimarisha vyama vya ushirika ili viwe chachu ya kilimo katika jamii
Akizungumza katika maadhimisho ya uzinduzi wa msimu wa kilimo yalifanyika kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Skimu ya Njage Mhandisi Kalobelo amesema tija kubwa ya sekta hiyo ni kpitia vyama vya ushirika kwani hata uazaji wa mazao unapitia vyama hivyo kama mkoa hawawezi kutegemea vyama kama havipo au vinakuwa na udhaifu.
Aidha amewataka wazalishaji wa pembejeo mkoani humo kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa kusambaza pembejeo kwa wakati na kuwasogezea wakulima huduma za kupata pembejeo kwa kufungua matawi kila wilaya ili wakulima waweze kuzalisha mazao bora na yenye tija.
Hata hivyo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mlimba na wananchi kwa matumizi mazuri ya fedha za mikopo ambazo zimeanza kuleta tija katika jamii ya watu wa Mlimba na hasa ambazo zimekuwa chachu kwenye maonesho mbalimbali yaliyofanyika kwernye uzinduzi wa wa msimu wa Kilimo wa mwaka 2020/2021
Kwa upande mwingine Mhandisi Kalobelo ametoa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni themanini na mbili laki sita na sabini kwa vikundi mbalimbali Wilayani humo ambazo zitakwenda kuongeza maendeleo ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa amemshukuru Katibu tawala wa mkoa na uongozi mzima wa mkoa kwa kukubali maazimsho hayo yafanyike wilayani humo kimkoa na wanachi wote wa wilaya ya Mlimba kwa kuzitendea haki fedha za mikopo walizopata kwani wameonesha taswira mwanzo mzuri wa safari ya maendeleo.

Mhandis Kalobelo akipanda mbegu za Mpunga katika moja ya kipando kijioji cha Njage Wilayani Mlimba tarehe 26/11/2020
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa