Aliyekuwa katibu wa Baba taifa hayati Julius Kambarage Nyerere Mh. Samweli Kasori amelishauri baraza la madiwani Kilombero kutumia fursa zao za uongozi kuhakikisha viwanda vilivyoanzishwa na Mwl Nyerere vilivyopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero vinaibuliwa na kuanza kufanya kazi.
Mh. Kasori ameyasema hayo alipokuwa amekaribishwa katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichokuwa kinapitia maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019, amekitaja kiwanda cha Mang’ula Mechanical Tools (M M T) kilichopo katika tarafa ya Mang’ula kilikuwa ni mojawapo ya viwanda vikubwa vinavyotegemewa ndani na nje ya Tanzania kwa utengenezaji wa vipuri.
Amewataka kutumia weledi wao kumuunga mkono Mh. John Pombe Joseph Magufuli katika kipindi hiki cha kuibua sekta ya viwanda nchini Tanzania kwa kuanzia ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya Kilombero.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa