Pichani juu: Mbunge wa jimbo la Mlimba akizungumza jambo kwenye baraza la kata
Jumla ya shilingi Milioni mia saba (700,000,000/=) zimetengwa katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 kwaajili ya ukarabati wa barabara zote zinazoingia kwenye sehemu mbalimbali katika jimbo hili la Mlimba.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Mlimba Ndg Gdwin Kunambi, alipokuwa akizungumza na watendaji wa kata pamoja na watumishi na viongozi wengine jana, katika kikao cha baraza la kata kilichofanyika jana katika ukumbi wa Cluster uliopo Mchombe katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba.
Akizungumza zaidi Ndg Kunambi amesema kuwa katika jimbo la Mlimba kuna jumla ya Kilometa zisizopungua 1000, ambazo ni nyingi sana ukilinganishwa na pesa aliyopewa lakini amejipanga kuhakikisha kuwa baadhi ya barabara zitajenga katika kiwango cha kufikika hasa katika kipindi cha Mvua ili kuweza kuwasaidia wananchi kufikia maazimio yao waliyojiwekea katika mikakati ya kujiletea maendeleo.
Aidha ameshauri katika kijiji cha mkuyuni ambapo kuna shida kubwa sana ya migogoro ya Ardhi, ameshauri kuwa ili kuweza kutatua migogoro hiyo, wamejipanga vyema kugawa Ardhi hiyo kisayansi kwani watagawa kwa makundi ya watu kuanzia ishirini huku Hati ya kumiliki Ardhi hiyo ikiwa moja tu ili kuepusha mipango ya kuuza ardhi hiyo inayofanywa na vijana ambao sio waaminifu na kuanzisha migogoro mbalimbali, kwani itawalazimu watu wote wanaomiliki eneo hilo kutia saini kwenye hati moja, ili eneo hilo liuzwe kitendo ambacho kitakuwa ni kigumu hivyo maeneo hayo yatabaki kuwa salama na wananchi wataendelea kurithishana kizazi na kizazi.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano kaliwa amewalaumu baadhi ya viongozi wa maeneo ya vijiji vya Halmashauri hiyo kuwakaribisha baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku ndio wanawasumbua sana wakulima, hivyo amesema kuwa atahakikisha uchunguzi unafanyika ili kubaini wale wote wanaowakaribisha watu hao na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kuepukana na matatizo hayo ambayo yanalalamikiwa sana kila mara.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa