Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg Ismail Mlawa (Aliyesimama) akiongea na wakaazi wa Mlimba
Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndugu Ismail Mlawa Mapema jana ametembelea maeneo ya Mlimba mjini katika moja ya ziara zake za kawaida kabisa katika wilaya ya mlimba ambayo ameteuliwa kuifanyia kazi mapema mwezi wa saba mwaka 2020.
Akizungumza na wakazi wa eneo la Mlimba ndugu Mlawa Amesema kuwa ameamua kufanya ziara hiyo, kwanza ili kuweza kuwatambua watu mbalimbali katika moja ya maeneo yake, lakini pili kuja kusikiliza kero mbalimbali za wananchi hao ili aweze kuanza kuzifanyia kazi.
Akijibu moja ya kero ya mwananchi aliyetaka kujua kuhusu kero ya kesi za mimba za utotoni kumalizwa na wazazi katika eneo hilo, amesema kuwa hilo ni swala ambalo halikubaliki kabisa na hiyo ni moja ya ajenda zake kwani amesikia kuwa eneo hilo linaongoza kwa vitendo hivyo vya kikatili na kuonya kuwa ikiwa mambo hayo yatafanyika kwa kipindi hiki basi wale wote watakaohusika na jambo hilo atawachukulia hatua kati za kisheria na kuwaasa wananchi kumpigia simu wakati wowote hata kama ni usiku wa manane kama kuna jambo lolote limetokea na linahitaji msaada wa haraka kutoka kwake.
Nae kaimu mkurugenzi Ndg Witness Kimoleta akitolea ufafanuzi juu ya upungufu wa walimu katika shule za mlimba hususan za pembezoni amesema kuwa kwa sasa Halmashauri wamekwishatuma maombi ya kuajiri baadhi ya walimu, hivyo kipaumbele kitakuwa kwa maeneo hayo ya pembezoni pindi kibali hicho kitakapotoka.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa