Pichani juu: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Ndg Dennis Londo akionyesha baadhi ya pikipiki walizopewa na TAMISEMI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kilombero Ndugu Dennis Londo mapema jana, amepokea Pikipiki ishirini ikiwa ni sehemu ya msaada kutoka TAMISEMI
kwa lengo la kuboresha na kuongeza nguvu kwa watumishi wa serikali kwa Halmashauri hiyo
Akiongea huku akionyesha tumaini jipya katika utendaji wa halmashauri yake,Ndg Londo amesema kuwa, Pikipiki hizo zilizosajiliwa kwa namba za DFP zitatumiwa
na Waratibu Elimu kata wa kwa matumizi ya ofisi ili kuweza kurahisisha shughuli za kiutendaji kazi kwa idara hiyo.
Aidha Bwana Londo aliongeza kuwa anayo furaha kubwa kupokea msaada wa Pikipiki hizo ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa katika shughuli za ndani ya
Halmashauri,kuboresha Elimu kwa kuzifikia shule kwa wakati na kutatua changamoto kupitia majukumu yao ya kila siku kwa shule zote za Msingi na Sekondari na
kuleta maendeleo kwa kiwango kikubwa kwa Taifa.
Pamoja na hayo pia alisema kuwa kwa sasa wamepunguza sehemu kubwa sana ya uhitaji wa pikipiki hizo, kwani uhitaji halisi ulikuwa ni Pikipiki 26, hivyo kupatikana
kwa pikipiki hizo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha utendaji huo huku wakiendelea kufanya utaratibu wa kupata pikipiki hizo sita kwaajili ya kata zilizo salia.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa