Pichani juu: mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Eng. Stephano Kaliwa akiongea na wafanyakazi wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, katika hafla ndogo ya utambulisho.
Mkurugenzi mtendaji mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Eng. Stephano Kaliwa, mapema leo amekutana na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwaajili ya kutambulishana na kuelezana changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuwa za mwanzo kukwamisha shughuli za kiutendaji katika halmashauri hiyo.
katika mazungumzo hayo, Eng. Kaliwa aliwataka watu wasiwe waoga katika kutekeleza majukumu yao, huku wakiwa wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.
Awali akitambulisha watendaji wa halmashauri hiyo, Afisa utumishi wa wilaya wa halmashauri hiyo bwana Abdul Mbimbi amesema kuwa, halmashauri ya wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa Halmashauri zenye ushirikiano mkubwa sana hivyo alimkaribisha Eng kaliwa na kumwambia ajisikie yupo nyumbani, huku akitambulisha watendaji hao kupitia Idara na vitengo vyao.
Aidha Eng. Kaliwa alijibu hoja mbalimbali za watendaji na wafanyakazi hao, kiasi cha kupelekea wafanyakazi hao kuridhishwa na majibu hayo huku wakiahidi kushirikiana nae kwa kadri iwezekanavyo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa