Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya yan Kilombero Injinia Stephano Kaliwa,amekabidhi pikipiki mbili aina ya boksa zitakazoweza kusaidia katika mradi wa uhilimishaji kama ilivyokusudiwa ili kuweza kuboresha Zaidi mradi huo.
Mradi huo wa uhilimishaji ulianza mwezi wa tano mwaka huu, ambapo tayari wafugaji 514 wameshapatiwa mafunzo mazuri juu ya suala zima la uhilimishaji.
Aidha mpaka sasa ng’ombe 17n wameshahilimishwa,japokuwa kwa mwezi huu wan tano uhilimishaji umekuwa mdogo sana, nah ii ni kutokana na maeneo mengi kujaa maji ila kuanzia mwezi wa sita uhilimishaji utaendelea kwa kasi, kutokana na maeneo mengi yatakuwa tayari yamekauka, pamoja na wafugaji wengi tayari wamepata hamasa ya kupandisha mifugo yao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii,Afisa uvuvi na mifugo Anethi Kitambi amesema kuwa wanashukuru kwa kupata usafiri wa pikipiki hizo mbili, huku halmashauri ikiendelea kuwafadhili mafuta(petroli) kwa ajili ya zoezi zima la uhilimishaji.
Pia amesema kuwa Wizara ya uvuvi na mifugo bado ina mipango mingijuu ya suala zima la uhilimishajina hii ni kutokana na kuwepo kwa wafugaji wane ambao tayari wamesomeshwa na kati ya hao wawili wamepewa pikipiki hizo na hao wengine halmashauri inaendelea na mchakato.
Hata hivyo uhilimishaji utazidi kuendeleaa ukiambatana na elimu bora ili kupunguza madume ya kienyeji yasiyokuwa na uzalishaji mkubwa na badala yake kutumia madume yaliyokuwa bora kama vile mbegu za saiwaa,fizian,hanshan,ng’ombe aina ya mpwapwa brid, bosinia na jese.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa