Pichani juu: Mkuu wa mkoa wa Morogoro mheshimiwa Kebwe Steven Kebwe akizungumza na wanafunzi wanaowakilisha wilaya mbalimbali za mkoa wa Morogoro katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro mheshimiwa Kebwe Steven Kebwe mapema leo amezindua michezo mbalimbali kwa shule za sekondari kwenye uwanja wa shule ya sekondari Ifakara.
Katika salamu zake za uzinduzi huo mheshimiwa Kebwe aliwasisitiza wanafunzi kuhakikisha kuwa wanafanya sana mazoezi hata baada ya kumalizika kwa mashindano hayo kwani mazoezi husaidia kuibua vichocheo vya kuchangamsha ubongo na hivyo kuwafanya waweze kufanya vema katika masomo yao ya kila siku.
Aidha aliwataka wakurugenzi wote katika mkoa wa morogoro, wahakikishe kuwa wanayafuatilia maeneo yote yanayoonekana kuwa yamevamiwa il hali yakiwa ni maeneo ya shule husika, kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanarudishwa kwenye shule husika hata kama mtu atakuwa tayari amekwishajenga ghorofa.
Katika hatua nyingine mheshimiwa Kebwe aliwasisitiza walimu wakuu na walimu wa michezo kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa kuwanoa vijana hawa ili waweze kuzoea kufanya mazoezi haya na ikiwezekana michezo hii hapo mbeleni iweze kuwa ajira zao.
Pia aliwakumbusha watumishi wote kuhakikisha kuwa wanafanya michezo kwa kila siku ya jumamosi ya pili ya mwezi kwani itaweza kuwasaidia watumishi kujikinga na magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza kama vile Kiharusi, kisukari, BP nk. Kama makamu wa Rais wa jamii ya muungano wa Tanzania alivyosema, na hii sio kwaajili ya kufuata tu maagizo ya serikali bali hata kuhakikisha kuwa wanapata afya na kupunguza athari mbalimbali za kiafya.
Mheshimiwa Kebwe pia aliwakumbusha wanafunzi hao wasije kucheza kwa chuki, kwakuwa michezo ni ajira, ushirikiano na ni furaha pia hivyo haina haja ya kugombana na kukubaliana na matokeo kwani asiekubali kushindwa si mshindani.
Mwisho aliwasihi kamati ya uchaguzi kuchagua wanamichezo kwa kuzingatia ujuzi na uwezo wao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kuweza kupata timu itakayoweza kuwakilisha vizuri mkoa wa Morogoro.
Chini: Matukio mbalimbali ya uzinduzi huo yakiwa pichani.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa