pichani juu: mkuu wa wilaya ya Kilombero akiongea na madiwani katika baraza la mawaziri
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo ametoa siku saba kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilombero ambao bado hawajahama kutoka Ifakara kwenda Mngeta wafanye haraka lasivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Ihunyo aliyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero baada ya madiwani kuhoji inakuwaje baadhi ya watumishi akiwemo Mkurugenzi wake Mhandisi Stephano Kaliwa kuendelea kuishi Ifakara ili mradi kuagiza watumishi Wa chini yake kuhamia Mngeta.
Mkuu huyo Wa wilaya alisema kuendelea kubaki Ifakara ni kukaidi maagizo ya Rais kwani hivi sasa watumishi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wanatakiwa kuishi Makao makuu mapya ya Mngeta ili kurahisisha kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema maelekezo yake yasipofanyiwa kazi ndani ya muda huo ataomba orodha ya Watumishi na kuwachukulia hatua bila kumuigopa mtu kwani katika jambo hili hakuna aliye mkubwa juu ya sheria.
Awali Madiwani wa halmashauri hiyo akiwemo Yusta Ndumba (Viti Maalum Kata ya
Masagati) na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo David Ligazio
walielezea kutoridhishwa na matumizi mabovu ya fedha za Halmashauri kunakofanywa na baadhi ya watumishi kwa ajili ya manunuzi ya mafuta kwenye vyombo vya usafiri wakitokea Ifakara kuja Mlimba pasipo kufuata Utaratibu.Ndumba alisema anashangaa mkurugenzi na baadhi ya watumushi kila siku wanafanya safari za kutoka Ifakara kuja Mngeta na kurudi Ifakara ili mradi huku madiwani wakipunjwa posho zao na kuhoji mamlaka hayo wanayatoa wapi watumushi hao?.
Wamesema haiwezekani baada tu ya kuhamia Mngeta posho za madiwani zipunguzwe wakati walishajitengea bajeti yao na kuhoji au Fedha zao ndizo zinapelekwa katika mafuta ya kuja na kurudi Ifakara.
Katika hatua nyingine Madiwani hao wamesema Mkurugenzi huyo amekuwa akiendesha Halmashauri pasipo kufuata utaratibu kwa kuwachukulia maamuzi ya kuwawajibisha watumishi kwa Kuwatishia kuwasimamisha kazi na kuwapa barua za onyo anapojisikia kufanya hivyo.
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa ndani Kutoka Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Steven Benedict akiwa katika kikao hicho
amesema ameshtushwa na hali hiyo ya malalamiko ya Madiwani juu ya kutokwenda vizuri kwa baadhi ya mambo hivyo katika hayo amewataka Madiwani kujenga ushirikiano kati yao pamoja na watendaji wa Halmashauri hiyo ili kwenda pamoja na kufanikisha shughuli za maendeleo kwa haraka.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa