Pichani juu Mkuu wa wilaya ya Kilombero Chief James Ihunyo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa Mikochini alipokwenda kuzindua chanjo ya Surua Lubera
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Chief James Ihunyo, mapema leo amezindua chanjo ya Surua Lubera katika eneo la kitongoji cha mikochini kata ya Namwawala.
Akizungumza katia uzinduzi huo Chief Ihunyo amewashukuru sana wananchi kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kiasi kwamba ilionekana kuwa kunahitajika huduma za ziada kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi hao.
aidha Ihunyo amesema kuwa kitongoji hicho kimepata upendeleo maalumu kwakuwa kimeonesha uhitaji mkubwa wa uhitaji wa chanjo kwani kuna watoto wengi sana na ni uhitaji wa serikali ni kuona wananchi wana afya njema kwaajili ya maendeleo ya Taifa hili, na kama ikitokea watoto wasipochanjwa basi kuna madhara makubwa ya kupooza pamoja na Surua kitu ambacho kinarudisha nyuma sana maendeleo ya Taifa hili.
Katika hatua nyingine Ihunyo amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kwa kuweza kusaidia upatikanaji wa dawa katika Wilaya hiyo kwani kwa sasa, hakuna kabisa tatizo la dawa katika eneo la wilaya yake kwani kila kituo cha Afya na hospitali zote kwa sasa kuna dawa za kutosha hivyo, amewashauri wananchi kwenda katika vituo hivyo kuimarisha Afya zao pindi wanapopata matatizo yoyote yale.
Nae mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Dokta Christina Guveti amewaasa wananchi kuwaleta watoto wao katika chanjo hiyo kwani haina madhara yoyote yale kiafya kwa mwanadamu, na hata kama ikitokea mtoto alipata chanjo mwezi uliopita sio mbaya akarejea tena kupata chanjo hiyo, kwani lengo la Taifa ni kuhakikisha kuwa watoto hao wanapata chanjo hiyo na wanakingwa na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwemo Surua, Lubela na Polio.
Dokta Guveti aliendelea kusema kuwa mtoto asipopata Chanjo ya Polio anaweza akapata ulemavu wa mwili hata upofu wa kudumu maisha yake yote, kitendo kitakachompa mzazi mzigo mkubwa wa kumlea mtoto huyo kwa kipindi hicho chote cha maisha ya mtoto huyo.
Chini ni Habari Picha
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa