Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imetekeleza mkataba wa utendaji kazi na usimamizi wa elimu kati ya Maafisa elimu Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa elimu Kata 16 zote za Halmashauri
Pamoja utekelezaji wa mkataba Maafisa Elimu kata 16 wamegaiwa vishikwambi ambavyo vitaenda kusaidia na kuraisisha utendaji wa Majukumu yao ya kitaaluma, utunzaji wa kumbukumbu pamoja na ufundishaji kwa njia ya kisasa.
Mwenyekiti wa Maafisa Elimu kata ameshukuru Uongozi wa Halmashauri kwa kusimamia zoezi la ujazaji wa Mikataba na kugaiwa vishikwambi na wamehaidi wataongeza ufanisi katika Utoaji wa Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa