Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg James Ihunyo (mwenye suruali nyeusi na shati nyeupe waliokaa) akiwa na baadhi ya viongozi wa MOROPEO na washiriki wengine mara baada ya kikao hicho.
SHIRIKA la wazee Morogoro(MOROPEO) limeipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya wazee kwani ilisahaulika licha ya kutolewa mwaka 2003.
Akizungumza katika uundwaji na uzinduzi Wa baraza la wazee ngazi ya halmashauri ya Wilaya ya Kilombero,Mkurugenzi Wa Moropeo Samson Msemembo alisema licha ya kuchukua miaka 16 tangu Sera ya Taifa ya wazee ilipotolewa na serikali mashirika ya wazee na wazee wenyewe kote nchini wameendelea kusukuma,kudai na kusubiri bila kukata tamaa kuundiwa mabaraza hayo.
Msemembo amesema hatimaye serikali sikivu ya awamu ya tano imepania kutekeleza na kuunda mabaraza katika ngazi zote na mfano ni halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na kudai kuwa hatua iliyofikia inatia moyo.
Alisema licha ya kuchelewa wanaendelea kupiga hatua kukamilisha uundwaji huo Wa mabaraza katika halmashauri zote na baadae kuuwezesha mkoa nao kuwa na baraza la wazee Mkoa na matumaini yao kukamilisha zoezi hilo hadi ngazi ya taifa kwa mwaka huu 2019.
Mkurugenzi huyo alisema pamoja na majukumu mengine baraza hilo la halmashauri litazungumzia na kutafuta ufumbuzi Wa kutatua kero na changamoto za wazee zilizo ndani ya uwezo Wa baraza hilo na kufikisha ngazi ya juu kwa ufumbuzi ulio juu ya uwezo wake.
Ametaja changamoto zinazogusa wazee ni pamoja na huduma za natibabu,pensheni na namna nyingine ya kipato,unyanyasaji Wa kikatili,huduma za usafiri,miundombinu,misamaha ya kodi na ushiriki na ushirikishwaji katika vyombo vya maamuzi.
Kwa upande wake Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema wazee ndio vyanzo vya busara katika maeneo mengi hasa kutokana na Vijana wengi kuwa na mihemko katika mambo yao.
Ihunyo amewataka wazee wilayani humo kutumia ujuzi Wa taaluma walizosomea katika kushauri mambo mbalimbali na serikali ya Wilaya itahakikisha wanaendelea kuishi kwa Amani na kutumiwa kwa ushauri pale watakapohitajika.
Ameziagiza ngazi zote kuhakikisha wazee hawasumbuliwi wanapofika kutoa malalamiko yao na pia kuandaliwa vitambulisho vya matibabu na kuahidi kuwa ofisi yake itaendelea kupokea ushauri Wa wazee wote bila kuwabagua.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe 52 kutoka katika Kata zote 26 katika halmashauri hiyo Veronika Wapalila alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Adam Komba makamu Mwenyekiti huku Alphonce Ngonyani akiwa Katibu na Msaidizi wake ni Asha Ligumba.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa