Pichani Juu: Ngombe mbalimbali wakipata maji kupitia Birika la kunywea maji huko Sagamaganga
Afisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya Kilombero Daktari Anette Kitambi, ameeleza kuwa wamekamilisha ujenzi wa birika la kunywea mifugo maji katika mnada wa Sagamaganga uliopo wilayani humo, ambao ukiwa ni moja ya mradi kati ya miundombinu iliyojengwa kwenye mnada huo mwaka 2016.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mapema leo asubuhi, Daktari Kitambi amesema kuwa, wamejitahidi kulifanikisha hilo ili waweze kuliboresha eneo hilo la mnada, pamoja nakutengeneza mazingira mazuri ya kiusalama kwa mifugo, ili kuondokana na adha ya magonjwa yatokanayo na kuwepo kwa hali mbaya ya mazingira, ambayo si salama kwa mifugo pamoja na wakazi waliopo karibu na eneo hilo la mnada.
Aidha Daktari Kitambi amesema kuwa, ili kulifanikisha jambo hilo, Halmashauri imeweza kutoa kiasi cha shilingi Milioni Thelathini (30,000,000) ili kuweza kukamilisha mradi huo ambao ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Sagamaganga na wote wanaozunguka eneo hilo ambao wanajishughulisha na shughuli za ufugaji.
“Sisi kama Halmashauri tumetoa shilingi Milioni Thelathini (30,000,000 ) ili tuweze kuukamilisha mradi ambao tumekusudia kuujenga,” amesema Daktari Kitambi.
Hata hivyo amewapongeza wananchi kwa kuonesha ushirikiano wa hali ya juu katika kuukamilisha mradi huo kwa kuchangia baadhi ya michango ikiwemo kutoa tofali zote za ujenzi, kuchimba shimo la choo, kuchimba mtaro wa bomba la maji kutoka kwenye vyanzo vyake ‘Resourse Center’ na kuchota maji ya kuendeshea shuguli zote za ujenzi pamoja na nyingine ndogondogo.
Sanjari na kuwepo kwa mradi huo wa Birika la kunywea mifugo maji, miradi mingine iliyopo katika eneo lile ni pampoja na Choo, kituo cha majiambacho kimetegemea zaidi mnara wa kuweka vihifadhia maji ‘simtank’ ambavyo tayari vihifadhia maji hivyo vipo, pamoja na pandishio.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa