Pichani juu: mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye huduma hizo za kupima afya na kupata tohara akipata huduma hiyo
Mradi wa furaha yangu uliozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Kebwe Steven Kebwe umezinduliwa mapema mwishoni mwa wiki hii katika kata ya Kiberege kwenye shule ya msingi Kiberege.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkuu wa wilaya ya Kilombero ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mradi huo, ndugu James Ihunyo amesema kuwa, kuna umuhimu mkubwa sana kwa wananchi wa kidatu na sehemu nyingine kwenye wilaya ya Kilombero kuweza kujua afya zao kwani kujua afya yako kutaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako.
Ndg Ihunyo alisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuweza kupata huduma hiyo ya uchunguzi wa matatizo mbalimbali kwaajili ya afya zao bure kabisa, kwani baada ya kupita huduma huyo hapo, hospitali nyingine hutoza pesa kiasi kadhaa, kwaajili ya kupata huduma hizo hivy amewasihi wananchi kuchangamkia furasa hiyo.
Awali Mganga mkuu wa wilaya ya Kilombero Dkt Samwel Lema alitanabaisha kuwa huduma zinazotolewa kuwa ni Upimaji wa VVU, uchangiaji wa Damu salama, elimu ya Lishe, upimaji wa BP uzito na urefu, Huduma za CTC na GBV, tohara kinga kwa wanaume pamoja na uchunguzi wa awali wa Kifua kikuu pamoja na magonjwa mengine ya ngono.
Nae mwananchi Julius Mangasini amesema kuwa, wamefurahishwa sana na uamuzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, kuamua kutoa huduma hizo katika kata yao ya kiberege kwani wamekuwa wakizisubiria huduma hizo kwa muda mrefu sana bila mafanikio yoyote, hivyo kuja kwa mradi huo katika eneo lao ni ukombozi mkubwa sana kwa jamii zao.
Kwa upande mwingine, shughuli hiyo ilifanikiwa sana, kwani watu wengi sana wamejitokeza kuhakikisha kuwa wanapata huduma mbalimbali kwa kadri itakavyowezekana.
Hapa chi ni Habari picha kuonyesha namna shughuli hiyo ilivyofanyika katika kata ya Kiberege siku ya Jumamosi tarehe 3/11/2018
Mganga mkuu a wilaya ya Kilombero, Dkt Samwel Lema akizungumza na wananchi waliojitokeza.
Baadhi ya wanachi wa kata ya Kiberege wakimsikiliza mgeni rasmi James Ihunyo.
Mgeni rasmi James Ihunyo akizungumza na wananchi wa kata ya Kiberege kwenye shughuli hiyo.
Shughuli za upataji huduma za Afya zinaendelea.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa