Pichani juu katibu mwenezi wa Chama cha mapinduzi Ndg Humphrey polepole akisaidiana kuzungusha mashine kukamua mawese na mmiliki wa kiwanda hicho mama Koleta Mikala.
Katika hali isiyo ya kawaida mradi wa TASAF katika wilaya ya kilombero, umekomboa kwa asilimia miamoja maisha ya mama Koleta Emilian Mikala ambae kwa sasa anamiliki kiwanda kidogo cha kukamua mafuta ya mawese katika eneo dogo alilolitenga nyumbani kwake huko maeneo ya Mbasa Ifakara.
Kwenye msafara wa kutembelea kiwanda hicho uliofanyika jana na Humphrey pole pole ambae ni Katibu mwenezi wa Chama cha mapinduzi, wakurugenzi wa halmashauri ya kilombero na Ifakara mji, viongozi pamoja na wananchi mbalimbali, mama huyo alisema kuwa iwapo atapatiwa mkopo mdogo wa kiasi cha shilingi milioni moja tu kuongeza manunuzi ya vifaa kadhaa vya kurahisisha shughuli yake basi angeweza kuomba kuondolewa kabisa katika orodha ya wenye uhitaji wa kusaidiwa pesa hizo.
Hata hivyo Ndg Polepole alimuombea mkopo huo na kuahidiwa kuupata mapema sana ili kuimarisha dhana ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa