Pichani juu: Injini wa umwagiliaji Injinia Romanus Myeye akiendelea na ukaguzi wa mradi wa umwagiliaji Kilombero
Afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Romanusi Myeye, amesema kuwa wamekamilisha uletaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo vitendea kazi vinavyohitajika katika ujenji wa mradi mpya wa pili wa mifereji ya umwagiliaji, ili kuweza kuukamilisha mradi wa ujenzi wa mfereji huo kwa ajili ya kupitishia maji huko mashambani.
Mradi huo ukiwa ni miongoni mwa miradi miwili ya umwagiliaji maji wa mita mia mbili na mita mia tatu na themanini, ambayo Halmashauri ilikusudia kuitekeleza kwa jamii ili kuweza kurahisisha kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wilayani humo, umebakiza mita chache tu ili kuweza kutumika na wakulima hao katika shughuli zao za kila siku za kilimo.
Akizungumza na muandishi wa habari hii mapema leo hii asubuhi ofisini kwake, Injinia Myeye amesema kuwa, kazi ya ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji maji wa mita mia tatu na themanini pamoja na kichepusha maji kimoja, unaendelea vizuri na umeshajengwa kwa sehemu kubwa isipokuwa bado mita ishirini na nne tu kukamilika.
Aidha Miyeye ameongeza kuwa, amejitahidi kuisimamia na kuifanya kazi hiyo kwa uhakika na ujuzi alionao, ili kuufanya mifereji uwe na muanguko mzuri unaotakiwa kitaalam kwa lengo la kurahisisha maji yaweze kutembea kiustadi kuelekea mashambani, kwaajili ya umwagiliaji huo.
“Nimejitahidi kuifanya kazi hii kwa uhakika na ujuzi wangu wote, ili kuhakikisha mfereji huo unaweza kupitisha maji kwa urahisi na kwa ustadi kuelekea mashambani kwaajili ya umwagiliaji,” amesema Injinia Myeye.
Awali Mkandarasi aliuchimba mfereji ambao haukuwa sahihi kitaalam kama ilivyotakiwa, kwa kuwa ulichimbwa kwa kwenda chini kupita urefu wa mashamba ambayo yanahitajika kumwagiliwa kwa kutumia mfereji huo, hivyo kupelekea kuvunjwa na kujengwa tena upya chini ya Afisa kilimo huyo Romanusi Myeye.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa