KILIO cha wakulima wa miwa wa nje katika maeneo mbalimbali nchini ni kuomba walipwe bei ya tani ya miwa kama wanavyolipwa wakulima Wa miwa wa Kilombero.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri Wa Kilimo na ushirika Omary Mgumba wakati akitoa taarifa ya wakulima wengine wakati Wa mkutano na wakulima wa wa miwa nje Wa Bonde la Kilombero.
Mgumba amesema kabla ya kuwatembelea wakulima Wa miwa Wa Kilombero aliwatembelea wakulima Wa miwa Wa Mtibwa na Mkurazi na katika kilio chao alisema wakulima hao waliomba walipwe bei kama wanayolipwa wakulima Wa Kilombero.
Naibu waziri huyo aliwapongeza wakulima wa miwa Wa Kilombero kwa kushirikiana na kiwanda kwa kuwa na bei nzuri ya tani ya miwa na kusema kuwa, bei nzuri ya miwa ndio faida kwamkulima kwani itamuinua yeye kiuchumi pia kukuza pato la taifa.
Alisema kwa sasa serikaliinatambua kwamba ukitaja zao la miwa macho yao yote yapo mkoani Morogoro hasawakulima Wa Kilombero na ndio maana viwanda viwili vya K1 na K2 vinadhamira yakuongeza ukubwa wa uzalishaji toka tani laki 120 000 na kufikia tani 250 000.
Naibu waziri huyo alisema katika kuendelea kumnufaisha mkulima Wa nje Wa miwa katika Bonde la Kilombero amemuagiza mkurugenzi Wa bodi ya sukari kumleta mtaalamu ili kusimamia uzito na utamu Wa sukari ambapo atashirikiana na mtu mwingine atakaechaguliwa na wakulima wenyewe lengo ni kushirikiana na kiwanda katika kuinua sekta hiyomuhimu.
Alisema baada ya kuhakikishiwa soko na mnunuzi hivi sasa kazi imebaki kwa mkulima kuzalisha kwa tija kwa kufuata kanuni bora za Kilimo ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Kuhusu suala la riba kubwa katika mabenki, naibu waziri huyo alisema wakulima wanakopa katika benki za kibiashara na ndo maana serikali ikawaanzishia benki ya Maendeleo yakilimo (ADB) ambapo ni benki maalum ya wakulima na pia wanashirikiana na benki za posta na NMB ambazo serikali ina hisa huku pia akisisitiza watumie benki ya TIB ambayo ina riba ndogo.
Amewataka wananchi katika bonde hilo kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya miwa na mpunga kwani taifa linawategemea na pia walime mazao ya muda mrefu kwani licha ya kipato pia watapata Fedha za kigeni na kuyataja mazao hayo kama korosho, kokoa, parachichina michikichi.
Kiwanda cha sukari Kilombero ndicho kinalipa bei nzuri ya miwa katika ukanda wote Wa Afrika na tani moja kwasasa inauzwa shilingi 101,000.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa