Pichani juu: Mkimbiza mwenge wa kitaifa LT. Josephine Mwambashi alipokwenda kutembelea chanzo cha maji katika kijiji cha miwangani
Mwenge maalum wa uhuru umekimbizwa mapema jana katika wilaya ya Kilombero ambapo jumla ya miradi saba imezinduliwa kuonwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Akizungumza na wananchi katika mradi wa mwisho kwenye Kijiji cha Miwangani, Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg. Hanji Godigodi amesema kuwa wanashukuru sana kwa miradi yote kwenda sawa kwani hakuna mradi hata mmoja uliokwama nah ii ni uthibitisho kuwa wilaya yake imefanya mkila ilichoweza kusimamia miradi ambayo imefanyika kwa kufuata taratibu zote za kipesa kwa kuzingatia thamani ya pes ana mradi tekelezwa.
Aidha Ndg. Godigodi amewashukuru wananchi kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kwenye kila mradi ambao ulipitiwa na mwenge ambapo hiyo imedhihirisha umoja uliopo katika Wilaya ya Kilombero ambayo imeonekana kuwa moja ya mfano bora katika Mkoa wa Morogoro.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa ambae ni mshiriki mwenza kwenye mwenge huu maalum wa uhuru amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamesaidia kwa Halmashauri yetu kufanya vizuri ni ushirikiano uliopo baina ya Halmashauri zote mbili hivyo amewataka watu wa kilombero kuendelea kushirikiana ili kusukuma gurudumu la maendeleo la wilaya ya Kilombero mbele.
Nae kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Ifakara Ndg Elias Shemtoe amewashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi na kuwaomba waweze kuitunza miradi yote ambayo imezinduliwa na mwenge huo kwani miradi hiyo ni mali ya wananchi na ipo kwaajili ya kuwahudumia wananchi wenyewe.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa