Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndugu James Ihunyo akijadiliana jambo na mkuu wa wilaya ya Ulanga ndugu Jacob Kassoma katika harakati za kuukabidhi Mwenge wilaya ya Kilombero jana katika kijiji cha Idete.
Mwenge wa uhuru jana umemulika miradi mitano ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, na kuacha ujumbe mzito unaohimiza watoto kusoma kwa bidii, katika kuyakomboa maisha yao.
Akitoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi wa eneo la Idete ambapo mwenge huo umepokelewa, kiongozi wa wakimbiza mwenge ndugu Charles Kabeho, amesema kuwa, ana imani kuwa kwa upande wa kilombero mambo yatakuwa mazuri sana kwani katika kutekeleza ujumbe wa mwenge kielimu mambo yatakuwa mazuri kwani inahitaji kila mzazi ajue masuala mazima ya kuchangia elimu kwaajili ya watoto wao.
Aidha ndugu kabeho amesema kuwa, wananchi wengi wamemuelewa vibaya Rais wetu Dkt John Magufuli kwa ile kauli yake ya elimu bure, na kusema kuwa suala la elimu bure si kutochangia maendeleo mengine madogomadogo ya shule, bali ni ule ulipaji wa ada ambayo serikali imejitolea kuwalipia wanafunzi wote, lakini suala la michango kama ya chakula kwa watoto hao pindi wanapokuwa mashuleni ni muhimu sana kwa afya za watoto wetu.
Kwa upande mwingine Mwenge huo wa uhuru, umetembelea miradi mitano ambayo ni pamoja na ofisi ya kijiji cha Igima pamoja na kugawa hati miliki za kimila, Nyumba za walimu za Kiburuburutu, Zahanati ya Njagi, Ghala la mazao la Londo pamoja na msitu wa Iwungi.
Tayari mwenge huo umekwishakabidhiwa kwa wananchi wa kilosa, huku ukiwa na mafanikio makubwa kwani miradi yote imefunguliwa na ile ya kutizamwa imefanikiwa na hakukuwa na dosari yoyote iliyopelekea kutokukamilika kwa miradi hiyo na kupelekea kutokufunguliwa.
Akitoa shukrani zake za dhati, mkuu wa wilaya ya Kilombero alisema kuwa, anawashukuru viongozi wadini, watendaji wote wa wilaya ya kilombero, Madiwani, vyama vya upinzani, wananchi kwa ujumla na wote walioshiriki, kwa kuweza kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ili kufanikisha shughuli hii.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa