Pichani juu: Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. Mwita Waitara akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero
Naibu waziri wa Tamisemi Mh. Mwita Waitara, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, kwa kutenga fedha kwaajili ya kukamilisha miradi mbalimbali, baada ya kuona moja ya mradi ambao ni shule, umekamilika vizuri kwa upande wa vyoo, madarasa pamoja na jengo jipya la Halmashauri namna linavyoendelea vizuri.
Mh. Waitara ametoa pongezi hizo jana, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, alipokuwa kwenye ziara yake katika Halmashauri hiyo, ambapo watu wengi walihudhuria wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa, walimu wakuu, wakuu wa idara pamioja na Mkurugenzi mtendaji na Mkuu wa Wilalaya hiyo.
Aidha Naibu waziri huyo amesema kuwa, licha ya kuwa na mafanikio hayo ndani ya Halmashauri hiyo, lakini pia zipo changamoto kwa baadhi ya shule kukosa walimu wa masomo ya hesabati na fizikia, hivyo kuwataka wahusika walioko katika sekta ya elimu, kulifanyia kazi jambo hilo haraka iwezekanavyo.
kwa upande mwingine Ndg Waitara amewataka wakuu wote wa idara wa masuala ya elimu, kuacha kukaa maofisini tu, na badala yake waende mashuleni kuangalia maendeleo na changamoto wanazokutana nazo wanafunzi, huku akiwakumbusha kuwa, Mkuu wa wilaya ana haki zote za kujua taarifa zote za miradi na maendeleo kwa ujumla, hivyo kuwataka Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya kushirikiana kwa kiasi kikubwa.
Vilevile Mheshimiwa Waitara amewataka watumishi wote wa uma kuwa na nidhamu ya kazi, waachane na tabia ya kujivuna, matumizi mabaya ya pesa za serikali na kujisifu kwenye kazi , hivyo kila mtu afanye kazi kwa nafasi yake na kwa kushirikiana, waache kufanya kazi kwa mazoea ili waweze kufika mbali zaidi kimaendeleo.
Hata hivyo Naibu waziri huyo amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli, kwa kuwa mfano bora katika kuleta maendeleo katika Nchi, kwani ameweza kufanya mambo mengi ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, ununuzi wa ndege na mengine mengi, hivyo kuwataka wananchi wote kuheshimu chama tawala kama mfano bora kwani kinawatoa watu wanaoleta maendeleo katika Nchi.
Sanjari na hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mh. James Ihunyo, amemshukuru Naibu Waziri huyo, kwa hotuba yake nzuri na kuahidi kuendelea kuyafanyia kazi yote aliyoyazungumza, ili kuleta maendeleo katika Nchi, kama katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyotaka.
“Ninakushukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa hotuba yako nzuri, kwani umeongea mambo mengi mazuri na nakuahidi kuyafanyia kazi yote uliyozungumza, ili kuweza kuleta maendeleo makubwa katika Wilaya yangu, amesema Mheshimiwa Ihunyo na kuwataka watu wote waliohudhuria kikao hicho, kuonesha ushirikiano katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa unaokuja.
Habari Picha: Baddhi ya matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye mkutano huo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa