• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Miundombinu
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

NAMNA HALMASHAURI YA MLIMBA INAVYOTEKELEZA SERA YA CHAKULA NA LISHE SHULENI

Posted on: January 29th, 2025


Utekelezaji wa Huduma ya Chakula na Lishe Shuleni umetokana na tamko la Sera ya Elimu na Mafunzo, ya mwaka 2014 kwamba Serikali itahakikisha kuwa huduma muhimu zikiwemo za chakula bora, mawasiliano, umeme, maji safi na salama na afya, zinapatikana katika shule na vyuo.

Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, ili kuhakikisha sera hii inatekelezwa kote nchini, miaka ya hivi karibuni iliandaa Mwongozo kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa suala la upatikanaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni. 

Ndani ya Mwongozo huo lengo kuu la Serikali katika kuhakikisha huduma hiyo inapatikana shuleni limeelezwa, kwamba tafiti zinaonesha kwamba huduma ya chakula na lishe inapopatikana shuleni, utoro kwa wanafunzi hupungua, usikivu huongezeka, mahudhurio ya wanafunzi huimarika, afya huimarika na kiwango cha ufaulu huongezeka.

Vilevile tafiti zinaonesha kwamba maarifa na umahiri unaotarajiwa kuwepo kwa mwanafunzi hupatikana pale ambapo huduma ya chakula na lishe inatolewa shuleni.

Hata hivyo, imebainika kwamba ingawa baadhi ya shule hutoa huduma ya chakula na lishe kwa siku zote tano za masomo na kwa wanafunzi wote, bado zipo shule ambazo hutoa huduma hiyo kwa wanafunzi ambao wamechangia na shule zingine hutoa huduma hiyo kwa siku chache za wiki, jambo ambalo sio kusudi la Serikali. 

Halmashauri ya Wilaya Mlimba ni miongoni mwa wadau watekelezaji na wasimamizi wa utekelezaji wa Sera za Serikali na katika suala hili la huduma ya chakula na Lishe shuleni, Halmashauri inajitahidi kadiri iwezavyo kuhakikisha huduma hiyo inapatikana katika shule zake zote za kutwa, hasa ukizingatia Halmashauri hii iko pembezoni na hivyo kwa kiasi kikubwa watoto hulazimika kutembea umbali wa kilomita kadhaa kwenda shuleni, hivyo ikiwa suala la upatikaji wa huduma hiyo shuleni halitawekewa mkazo zaidi ni wazi nia ya Serikali ya kuwa na Taifa lenye uchumi unao kua kwa kasi kupitia kuwa na jamii yenye afya tele haitafikiwa.

Kwa kweli Halmashauri ya Mlimba ni mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni. Halmashauri hii ina jumla ya shule za msingi 99 za serikali na huduma ya chakula na lishe inatolewa kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wote, katika siku zote  tano za wiki.

Halmashauri iliwezaje kufanikisha hili? Ndugu Msee Sokoyet Kivuyo, ambaye ndiye Msimamizi wa Utekelezaji wa shughuli za lishe katika Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, anasema Halmashauri kupitia klabu za lishe zilizopo shuleni, imekuwa ikipenyeza elimu ya umuhimu wa kuwepo kwa huduma ya chakula na lishe shuleni, jamii imeelewa na sasa inaunga mkono hilo.

Ndugu Kivuyo anasema, njia wanazotumia kufanikisha upatikanaji wa huduma hii ni kupitia michango ya wazazi, kulima bustani za mbogamboga na mashamba shuleni.

“Miongoni mwa shule 99 ambazo Halmashauri inazimiliki, shule 88 zina bustani za mbogamboga na mashamba ya mpunga na mahindi. Shule 11 zenyewe huotesha mbogamboga kwenye viroba na makopo kwa sababu hazina maeneo kwa ajili kilimo na kwa upande wa chakula cha nafaka, wazazi na walezi wa wanafunzi huchangia”. 

“Mchicha, Chainizi na Figiri ndio mbogamboga ambazo hulimwa sana kweye bustani za shuleni na kwa upande wa chakula, mchele na mahindi”. Alifafanua ndugu Kivuyo.

Naye mmoja wa walimu wa shule za msingi za halmshauri ameeleza kwamba kuwepo kwa chakula shuleni kumepunguza sana utoro wa rejareja, kunatoa muda wa kutosha kujifunza na kufundisha, na kumeleta umoja na mshikamano baina ya wanafunzi kwa wanafunzi, na walimu na wanafunzi.

“Lakini sisi tunapambana kuhakikisha huduma ya chakula na lishe inapatikana shuleni, sio tu ili wanafunzi wafaulu masomo yao bali tunaamini kwamba hata baada ya kuhitimu masomo, elimu hii itawasaidia wanafunzi wetu kuendelea kumudu maisha yao wawapo uraiani”. Aliongeza kusema mwalimu huyo.

Ni dhahiri kwamba upatikanaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni unachangia sana katika kuinua taaluma na ufaulu katika shule za msingi za Halmashauri ya Mlimba. Takwimu zinaonesha hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi ndani ya Halmashauri ni kuanzia asilimia 100 na kuendelea, na hiyo ni tangu mwaka 2020, Halmashauri hii ilipo anzishwa.

Wito wangu ni kwamba Halmashauri zingine za pembezoni ambazo huenda bado zina sua sua katika utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni, zijifunze toka Halmashauri ya Wilaya Mlimba, ili kwa pamoja tuwe imara katika kufanikisha utekelezaji wa suala hili la huduma ya chakula na lishe shuleni, kwa asilimia 100 na zaidi.

Imetolewa na,

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

29.01.2025



Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA MWENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI February 13, 2025
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA MWEZI DESEMBA 2024 January 07, 2025
  • KIUNGANISHI (LINK) YA MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI MWAKA 2024 January 05, 2025
  • KIUNGANISHI (LINK) CHA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA UPIMAJI WA DARASA LA NNE MWAKA 2024 January 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI JAMARY AWAPOKEA MADAKTARI BINGWA WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    June 10, 2025
  • MHE. WAZIRI WA MAMBO YA NJE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MLIMBA DC

    June 04, 2025
  • MLIMBA DC YAPOKEA VITABU 13,607 KWA AJILI YA SHULE ZAKE ZA SEKONDARI

    May 30, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPOKEZI YA VIFAA VYA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Kupata Madarakani au cheo hakukufanyi kujua kila kitu. Maneno ya hekima kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Mhe. Dkt Doto Biteko
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa