Pichani juu: Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa akikagua eneo la ujenzi wa ofisi za Halmashauri pembeni yake ni Mhandisi wa Ujenzi Injinia Baraka
Ofisi mpya ya Halmashauri ya wilaya ya Mlimba imeanza kujengwa kwa kasi kubwa kwa kuanza kuchimbwa msingi kwaajili ya majengo yake ambayo yatakuwa ni ya Ghorofa katika eneo la Itongoa katika kata ya Mngeta wilayani Kilombero, hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mhandisi Stephano Kaliwa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Habari hii mapema leo asubuhi katika kuzungumzia maendeleo ya ujenzi huo.
Mhandisi kaliwa ameongeza kuwa kwa pesa hizo walizozipata zinaweza kukamilisha ujenzi wa jengo hilo katika hatua za awali (Structure) na kuliezeka juu ili kuweza kufanya ukamilisho wa ujenzi huo katika hatua za mwanzo ambazo zitakuja kufuatiwa na hatua za pili mara tu hatua hiyo ya mwanzo itakapokamilika.
Aidha Mhandisi Kaliwa ametanabaisha kuwa, shughuli ya ujenzi huo itakwenda kwa haraka sana ili kuweza kuendana na kasi ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ambae anasisitiza mambo yanayohusiana na serikali na yenye kuleta tija kwa wananchi yaweze kufanywa kwa haraka ili kusaidia utoaji bora wa Huduma kwa wananchi wa maeneo husika.
Nae Afisa anaeshughulikia masuala ya ujenzi wa Halmashauri hiyo, mhandisi Baraka Lolila amesema kuwa ujenzi huo kwa namna yoyote ile ulitakiwa uanze mapema kwasababu tayari halmashauri imekwishapokea kiasi cha shilingi Bilioni moja 1,000,000,000/= kutoka serikali kuu na mchakato wa kumpata mkandarasi ulikwisha na amepatikana Suma JKT kama mkandarasi ambae kwa sasa ndie ameanza kazi ya uchimbaji wa msingi wa mwanzo katika ujenzi huo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa