Pichani juu: mkulima akiangalia baadhi ya panya waliokufa kwa kushindwa kutoka kwenye ndoo yenye maji, baada ya kutumbukia wakitafuta maji
Panya waliokuwa wanaendelea kubungua mahindi na kuharibu mpunga katika skimu ya umwagiliaji ya kata ya Mchombe na Njage, wamekwishaanza kupatiwa ufumbuzi kwa kubuniwa mitego mbalimbali na sumu ambazo zimekwishaonyeshamatokeo chanya katika kuwaangamiza panya hao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mhandisi Romanus Myeye amesema kuwa, tayari wamekwishaanza kutumia uvumbuzi huo ambapo umekwishaangamiza panya wengi sana.
Mhandisi Myeye amesema kuwa katika kuwaangamiza panya hao mkulima anatakiwa ategeshe ndoo yenye maji chini ya udongo, kisha unazungushia pumba kwa pembeni ya maji hayo, hapo panya atakula sana na baada ya kula atabanwa sana na kiu, na kwakuwa ataona maji na yapo, atayafuata na kuingia ndani, sasa akishaingia kutoka hatoweza.
Kwa upande wa matumizi ya sumu aina ya Zinc Phosphate, mhandisi Myeye amesema kuwa, tayari wamekwishawaelekeza namna ya kuichanganya na pumba na tayari wamekwishapunguza panya wengi sana na hatimae, wameanza kupata nafuu na mashamba yao.
Nao wananchi kwa nyakati tofauti wamezishukuru jitihada za Halmashauri kwa kuweza kuwasaidia kuwaangamiza wanyama hao, kwani wamekuwa kero kubwa sana katika maendeleo ya maisha yao kwenye kilimo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa