Pichani juu: mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg Loata Sanare (katikati) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba (Hawapo pichani) Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg Ismail Mlawa na Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobero
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loatha Ole Sanare ameendelea na ziara ya kutembelea wilaya mbalimbali mkoani humo, akizindua, kukagua miradi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.
Akiwa ziarani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba mapema jana, Ndg Sanare ametembelea katika Hospitali ya wilaya hiyo inayojengwa katika eneo la makao makuu ya Halmashauri hiyo iliyopo katika kata ya Mngeta eneo la Itongoa.
Ndg Sanare amesema kuwa, serikali haina fedha za kuongeza katika ujenzi wa hospitali zote za wilaya tofauti nchini ikiwamo hii ya wilaya ya Mlimba, endapo tu kutakuwa na matumizi mabaya ya fedha hizo, kwani kuna miradi mingi inakwenda kutekelezwa nchini.
Akizungumza Zaidi Ndg Sanare ameutaka uongozi wa wilaya ya Mlimba, kuhakikisha wanakuwa na mpango kazi mahususi ili kuwe na urahisi wa kufuatilia ujenzi huo kwa kila hatua inayofikiwa.
Katika hatua nyingineNdg Sanare amemtaka mkandarasi wa hospitali hiyo kuwatumia wananchi wa wilaya hiyo katika shughuli ndogondogo zinazo hitaji nguvu kazi ili waweze kunufaika na mradi huo na sio kuchukua watu wa sehemu nyingine kama ambavyo amefanya kwa baadhi ya kazi.
‘’Mkandarasi kitu kingine ninavchotaka kukushauri ni kuwa fedha zipo, hauna sababu ya kuchelewa hapa kuna watu wa kutosha wape kazi wafanye na wao wafaidike sio unakwenda kuchukua watu wa Ifakara, Si ndio jamani?’’ Alimaliza kwa kuuliza.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa