Pichani juu: mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Martine Shigela akisisitiza jambo wakati akiongea na madiwani, watumishi na wananchi katika kikao cha baraza maalum la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Martine Shigella mwishoni mwa wiki hii katikabaraza maalumu la kujadili ripoti ya mkaguzi mkuu, ameipongeza Halmashauri yawilaya ya Mlimba kutokana na umakini mkubwa kwenye matumizi ya fedha zakekatika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Katika hotuba yake hiyoamesema kuwa amefurahishwa sana na namna ambavyo Halmashauri hiyoinashughulikia suala hilo lakini pia akashauri kuwa ni vema sasa wakahakikishawanajenga miradi hiyo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani tu na si kutegemeawafadhili, wananchi au pesa kutoka serikali kuu, kwani itapendeza sana sikumoja Halmashauri ikisimama na kusema kuwa imefanikiwa kujenga mradi Fulani kwakutumia fedha za ndani kwa 100%, na si kuchanganya pesa za mapato ya ndani, CSRwala mchango wowote kutoka kwa wananchi na kama wakiweza kufanya hivyo basiHalmashauri itakuwa ni ya mfano katika Halmashauri zote katika mkoa huu waMorogoro.
Aidha katika hatua nyingine Mh. Shigella amesisitiza kuwa miradiitakayojengwa hapa iwe ni ile ya kuwasaidia wananchi, mfano kujenga magodauniyatakayosaidia kuhifadhi mpunga wa wananchi n ahata ikitokea kuna mkwamo waaina yoyote ilebasi serikali ipo tayari kuwasaidia ili kuhakikisha kuwa mamboyanakwenda sawa.
Nae mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mhe. Innocent Mwangasa amesema kuwamaagizo yote waliyopewa na mkuu wa mkoa wameyapokea na watayafanyia kazi nasiku si nyingi, kikubwa ni ushirikiano tu ambao amesisitiza kuwa utakuwepo ilikuweza kufanikisha shughuli hii.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimbamhandisi Stephano Kaliwa amesema kuwa ameyapokea maagizo hayo na walikuwa wapokwenye mchakato wa kulifikiria hili hivyo mkuu wa mkoa amekuja kukazia na hivyowatajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa agizo hilo linapewa nafasi yamwanzo ili kuweza kuwapa wananchi huduma wanazostahili katika wakati sahihi.
Habari picha.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa