Pichani juu: mwekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Ndg David Ligazio akisisitiza jambo kwenye baraza hilo
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Inatarajia kupata zaidi ya
shilingi bilioni.46.7 kutoka vyanzo vyake mbalimbali kwa ajili ya kuendesha shughuli za Halmashauri na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2020/2021.
Akizungumza katika kikao cha bajeti kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo David Ligazio amesema kiasi hicho shilingi bilioni 4 zitatokana na mapato ya ndani.
Ligazio amebainisha kuwa vipaumbelea walivyojiwekea ni pamoja nakufanikisha jatika sekta za kilimo,mifugo, Afya na Elimu ambapo katika Elimu imetengwa kiasi cha sh Mil 400 kwa ajili ya uboreshaji wa niundombinu ya Elimu ni kutokana na wimbi kubwa la watoto wanaoanza elimu ya Msingi
Amesema kiasi cha shilingi milioni 200 katika sekta ya Afya huku akisema fedha hizo ziguse
moja kwa moja katika miradi ya kuwanufaisha wananchi badala ya
kutumia fedha nyingi kwenye matumizi ya kawaida..
Akizungumzia miradi ya kimkakati,Ligazio aliitaja kuwa ni pamoja na ujenzi Wa skimu za umwagiliaji Bonde la Kisegese,Ujenzi Wa hospitali ya halmashauri ya Wilaya ba Ujenzi Wa ofisi ya halmashauri ambapo kuasi cha shilingi bilioni 15.1 kimetengwa.
Hata hivyo baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo,baadhi ya wadau walisema imeegemea zaidi upande mmoja Wa tarafa za Mngeta na Mlimba na kuacha tarafa za Mang'ula na Kidatu wakati hadi sasa maamuzi ya kutenganisha halmashauri mbili bado kufanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema bajeti hiyo imegusa zaidi miradi katika Tarafa ya Mlimba huku Tarafa za Kidatu na Mangula zikiachwa hali ambayo amesema hali ni upendeleo na kwamba japo hilo sio zuri hivyo ameitaka halmashauri hiyo kutenda haki katika maeneo yote kwani mpaka sasa bado maeneo hayo yanaitikia katika Halmashauri ya Kilombero.
Ihunyo alisema kweli sasa inajulikana kutakuwa na halmashauri za Mlimba na Mji Ifakara na hatua za awali zimefanyika ila nado maamuzi ya juu hayajafanyika ili kuruhusu halmashauri hizo kujitegemea hivyo kwa sasa tarafa zilizobaki zina haki ya kupata miradi kwani bado zinaitikia halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hilda Mahimbali amelishukuru baraza hilo la madiwani kwa kuonesha ushirikiano wa kupitisha Bajeti hiyo kwani kwani itarahisisha utoaji huduma kwa wananchi waliowapa dhamana ya kuwawakilisha.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa