SHIRIKA la Plan InternationalIfakara limetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 31,400,000 kwa ajiliya kuboresha sekta ya Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Makabidhianohayo yamefanyika juzi katika ofisi ya halmashauri hiyo toka kwa Meneja Wa PlanInternational Ifakara Majani Rwambali kwenda kwa mkurugenzi Mtendaji Wahalmashauri hiyo Dennis Londo.
Akikabidhivifaa hivyo Rwambali amesema wao kama shirika wameanza kushirikiana nahalmashauri hiyo katika kutekeleza mradi Wa Huduma zinazotolewa nje ya Kituocha tiba(Mkoba) toka mwaka 2016 na mojawapo ni kusaidia vifaa katikavituo vya tiba 48 katika halmashauri hiyo.
Rwambalialitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni pamoja na Microscopes 5,mizani ya kupimiawatu wazima 48,mizani ya kupimia watoto 48,mashine za kupimia BP 48 naStethoscopes 48 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 31.4.
Menejahuyo Wa Plan amesema kuwa misaada hiyo licha ya kupitia kwao imetolewa kwaufadhili Wa shirika LA Daiichi-Sankyo toka nchini Japan na kusema kuwa shirikalao litaendelea kuisaidia halmashauri hiyo kwa kufika katika vituo hivyo 48kila mwezi.
Kwaupande wake mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri hiyo Dennis Londo aliwashukuruPlan na Daiichi- Sankyo kwa msaada huo ambao kimsingi wanaendelea kuonyeshawapo sambamba na halmashauri katika ushirikiano Wa mambo mbalimbali.
Londoamesema vifaa vilivyotolewa sio haba hasa kwa halmashauri ambazo zinarasilimali chache na majukumu mengi na anaamini uwepo Wa vifaa hivyoutarahisisha hali ya utendaji Wa watumishi wao katika vituo vya Afya nazahanati zote hasa zilizopo katika mradi.
Mkurugenzihuyo amesema anaamini vifaa hivyo vitaboresha Afya za watu hasa Afya ya mamawajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano na amewahakikishia wafadhilihao kwamba vifaa hivyo vitatumika kwa kadri ya malengo ya mradi huo katikakuboresha Afya za wananchi.
Naemganga mkuu Wa halmashauri hiyo Dk Samwel Lema alisema licha ya kuwasaidia kwakuwapatia vifaa hivyo pia shirika hilo mwaka jana waliwapatia gari ambayoimesaidia katika kuboresha huduma za chanjo kwa mama na watoto kwani awalikiwango cha chanjo kilikuwa chini ya asilimia 70 lakini sasa huduma ipo kwaasilimia 90.
Hatahivyo Mratibu Wa huduma za chanjo katika halmashauri hiyo Nendaeli Malugualisema baada ya kupatikana kwa vifaa hivyo ana imani kila Kituo kitakuwa nakifaa cha vipimo kwa akinamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitanona vifaa vitapelekwa katika kanda zote tatu za mradi ambazo ni Mang'ula,Mngetana Mlimba.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa