Pichani juu: Afisa Elimu vifaa, akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kiberege ambao wameweka kambi na wanafunzi wa darasa la saba.
Shule ya msingi kiberege iliyopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero wiki mbili zilizopita, imeanza kambi ya wanafunzi wake kwaajili ya maandalizi ya mtihani wa darasa la saba.
Wakizungumza na Afisa elimu vifaa ndugu Said Kivufu ambae aliwatembelea ili kukagua kambi hiyo inavyoendelea, mwishoni mwa wiki hii, walimu ambao wameamua kuweka kambi na wanafunzi hao kwaajili ya kuzidisha uelewa wa ziada kwa wanafunzi hao walisema kuwa, tayari wameanza kambi hiyo na wanatarajia kuendelea na mpango huo mpaka pale watakapoona watoto wao wameiva kwaajili ya mtihani wao wa mwisho.
Aidha walisema kuwa, mambo ambayo huwasaidia watoto hao ni pamoja na, kusaidia kumalizia mada ambazo bado kwa mujibu wa mitaala ya elimu, kuwafundisha namna ya kuelewa maswali na kuyajibu kwa ufasaha, kutoa maswali na kuwasaidia kujibu pale wanapokosea, n.k
Kwa upande wake ndugu kivufu alisema kuwa ni jambo bora sana kuamua kuweka kambi hii kwani utakuwa ni msaada mkubwa sana kwa watoto hao ambao ikiwa wataachwa kama walivyo, watakosa kufanya vizuri.
Aidha alisisitiza kuwa ni vema sana kutumia mbinu mchanganyiko kidogo kama vile,muhamo wa luwaza pamoja na kufundisha mbinu tofauti kwenye swali moja pindi wanapowafanyia masahihisho wanafunzi hao.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa