VIJJI vitatu vya Signali, Sululu na Sakamaganga vilivyopo kata ya Signal wilaya ya kilombero mkoani Morogoro vimemaliza mgogoro mkubwa wa mipaka yake na hivyo kuwa kwenye fursa ya kunufaika na mradi wa upimaji na urasimishaji ardhi (LTSP).
Wilaya za Kilombero,Malinyi na Ulanga ni wilaya tatu zilizochaguliwa kutekeleza zoezi la upimaji na urasimishaji wa ardhi kwa majaribio katika mkoa wa Morogoro lengo kuu likiwa ni kupanga matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro na ugomvi baina ya wakulima na wafugajii.
Akitoa taarifa hiyo kwa katibu mkuu wa ardhi,Nyumba na maendelea ya makazi Doroth Mwanyika aliye ziarani wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,kupitia mkutano na wanakijiji cha kwenye mkutano wa wanakijiji cha Sakamaganga,Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo alisema mgogoro huo umemalizika baada ya vikao Zaidi ya vitano vilivyofanyika na wanavijiji hao kwa nyakati tofauti.
Alisema kuwa kutokana na mgogoro huo,timu ya wapimaji kutoka mradi wa upimaji na kurasimisha ardhi ilishindwa na kuendelea na zoezi lake la upimaji ardhi ya vijiji hivyo.
“Nafurahi kuutangazia umma mbele yako katibu mkuu, kuwa ule mgogoro wa mipaka wa vijiji vitatu umeisha na kwahiyo lile zoezi lililosimama kwa muda la upimaji wa ardhi na baadaye kuurasimisha ardhi linaweza kuendelea,”alisema Ihunyo.
Ihunyo aliendelea kusema kuwa ofisi yake iko kwenye hatua ya kumalizi mogogoro mwingine wa ekari 60 baina ya wawekezaji binafsi na Kijiji cha sekamagamba ambapo timu ya wataalam wa sheria wakishirkiana na maafisa ardhi wa manispaa wanashughulikia.
“Nimeshaagiza timu ya waataalam wa sheria kutoka ofisi yangu washirikiane wa maafisa ardhi kulishughulikia tatizo hilo ili haki iweze kutendeka kwa pande zote mbili za mgogoro,”alifafanua mkuu huyo wa wilaya.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewahakikishia wananchi wa vijiji jirani na barabara itokayo kidatu mpaka Ifakara kuwa hakuna mkazi nyumba yake itabomolewa kupisha upanuzi wa barabara bila kulipwa.
Alisema zoezi liko wazi na tathmini inaendelea kuafanya na timu ya wataalam kutoka wakala wa barabara(TANROAD) wakishirikia na wa maeneo husika inapopita barabara hiyo ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akihutubia wananchi hao,Katibu mkuu wa wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Dorothy Mwanyika aliwataka wanavijiji hao kutumia fursa mbalimbali zinazotopatikana kupitia mradi wa upimaji na urasimisha ardhi ili kujiletea maendeleao ngazi ya familia,Kijiji na taifa kwa ujumla.
Alisema migogogo ya ardhi ni chanzo kikubwa cha kudorora kwa maendeleo maeneo husika kutokana na muda mwingi kutumika kukashughulika kutatua migogoro hiyo na kutumia muda mchache kwenye shughuli za maendeleao.
“Nawashukuru kwa kuwa tayari kumaliza migogogro na hivyo nawaomba kutumia fursa za mradi huu ili kuweza kujiletea maendeleao yenu wenye kwenye kaya,Kijiji na hata taifa kwa ujumla.Ardhi yako ikipimwa, thamani yake inaongezeka maradufu,” Mwanyika alisema.
“Natoa mwito kwa timu ya wapima kuanza zoezi hili mara moja ili kukamilisha zoezi katika vijiji hivyo vitatu na hatimaye waweze kukabidhiwa hati zao za kimila baadae.Mtoe ushirikiano kwa wapimaji ili zoezi liweze kwenda kwa haraka Zaidi.
Kwa upande wake mkazi wa Kijiji hicho Isa Lupia alimwomba katibu mkuu kuhakikisha kuwa zoezi la upimaji lingalie pia namna gani wanavijiji watanufaika na miradi iliyopo ndani ya eneo la Kijiji chao ikiwemo mgodi wa machimbo yam awe.
Alisema imefikia wakati na wao kama wanakijiji kunufIKA miradi mikubwa kama hiyo imayoendelea Kijiji hapo kama ujenzi wa shule na zahanati kama maeneo mengine wanavyonufaika na miradi kama hiyo.
Mwisho
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa