Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Mohammed Ramadhani juu pichani, ifuatayo ni taarifa fupi ya hali ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya kilombero
kama alivyoongea na Afisa habari wa Halmashauru hiyo ndugu ISLAM MPOSSO
1.0 Hali ya chakula Wilaya ya Kilombero Feb 2018
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi 2012 Wilaya ya Kilombero ina wakazi wapatao 407,880 na jumla ya kaya 94,604. Ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni asilimia 2.4, hivyo kadirio la idadi ya watu kwa mwaka 2016/17 ni Halmashauri ya Wilaya kuwa na watu 344,410. Mahitaji halisi ya chakula mchanganyiko kwa mwaka itakuwa ni tani 138,194 (tani 124,374.6 za chakula aina ya wanga na tani 13,819.4 za chakula aina ya utomwili). Utekelezaji wa malengo/uzalishaji 2016/17 ni tani 572,664 hivyo ikiwa ni ziada ya tani 434,470.Hivyo Halmashauri ina chakula cha kutosha na hakuna tishio la njaa katika ujumla wake.
1.1. Upatikanaji wa Chakula na Bei zake
Upatikanaji wa chakula ni mzuri kwa ujumla, isipokuwa bei ya baadhi ya vyakula hasa mchele imepanda katika kipindi hiki kwa sababu baadhi ya maeneo mengi ya nchi hayakuzalisha chakula cha kutosha. Hali hii imesababisha wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kuja kununua mchele kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero lakini hali iko tofauti katika zao la mahindi bei imeendelea kupungua hadi kufikia Tsh.10,000 kwa debe kwa bei ya juu na chini ni 5,500. Tazama jedwali No.1 hapo chini:-
Jedwali Na.1: Bei ya Mazao Sokoni.
Na
|
Aina ya Chakula
|
Upatikanaji wa
Chakula Sokoni |
Kinakopatikana
|
Bei ya
chini kwa kilo/Tsh. |
Bei ya
juu kwa kilo/Tsh. |
|
Kinapatikana/
Hakipatikani |
Ndani ya
wilaya |
Nje ya
Wilaya |
||||
1
|
Mahindi
|
Kinapatikana
|
√
|
|
306
|
556
|
2
|
Mpunga
|
Kinapatikana
|
√
|
|
533
|
867
|
3
|
Ngano
|
Kinapatikana
|
|
√
|
2,000
|
2,500
|
4
|
Mtama
|
Kinapatikana
|
√
|
√
|
1,800
|
2,000
|
5
|
Ulezi
|
Kinapatikana
|
|
√
|
1,500
|
2,500
|
6
|
Uwele
|
Kinapatikana
|
|
√
|
2,000
|
2,500
|
7
|
Makopa
|
Kinapatikana
|
√
|
√
|
1,600
|
2,200
|
8
|
Mhogo mbichi
|
Kinapatikana
|
√
|
|
650
|
1,150
|
9
|
Viazi vitamu
|
Kinapatikana
|
√
|
√
|
950
|
1,150
|
10
|
Viazi Mviringo
|
Kinapatikana
|
|
√
|
1,000
|
1,250
|
11
|
Ndizi
|
Kinapatikana
|
√
|
|
850
|
1,050
|
12
|
Maharage
|
Kinapatikana
|
|
√
|
1,800
|
2,400
|
13
|
Mikunde mingine
|
Kinapatikana
|
√
|
√
|
1,500
|
1,800
|
Nb. Mchele bei ya chini ni Tsh.1,450 na ya juu ni 2,000 kwa kilo.
Unga wa Mahindi bei ya chini ni Tsh. 1,000 na ya juu ni 1,250 kwa kilo.
Halmashauri ya Wilaya inaendelea kuhamasisha Wananchi kuwa na tabia ya kuhifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya mwaka mzima kwa:-
Kutoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula.
Kupanua wigo wa kulima mazao mengine badala ya chakula badala ya kutegemea zaidi zao la mpunga.
Kuhimiza wananchi kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na yanayostahimili ukame.
-Kuhimiza wakulima walioko katika maeneo ya umwagiliaji kuendelea kuzalisha zaidi ya mara moja kwa mbinu ya mazao mchanganyiko pale inapoonekana maji hayatoshelezi kulima mpunga eneo lote.
1.2. Hali ya Hewa
Kwa msimu 2017/18 mvua zimeanza kunyesha kwa muda muafaka, japo hazina matawanyiko mzuri lakini tayari kazi muhimu za maandalizi ya mashamba, upandaji na utunzaji wa mimea iliyopo shambani unaendelea. Katika mwezi Februari kumekuwa na upungufu mkubwa wa mvua kulikopelekea baadhi ya maeneo yaliyopandwa zao la Mahindi kuathirika kwa kukosa unyevu wa kutosha kuzalisha. Tazama jedwali Na.2. linaloonesha mwanguko wa Mvua kwa kituo kilichopo bomani;-
Jedwali Na.2 Mwanguko wa Mvua - Msimu 2017/2018 hadi Feb 25 2018
Mwezi
|
Sept
|
Octoba
|
Nov
|
Disemba
|
Januari
|
Februari
|
Jumla mm.
|
0 |
0 |
49.8 |
137.9 |
261.4 |
2.7 |
Idadi ya Siku
|
0 |
0 |
6 |
5 |
9 |
1 |
2.0. Hali ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula
Utekezezaji wa malengo ya Kilimo kwa mwaka umekuwa ukiathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa mvua ambazo zimekuwa si zauhakika wa kutosheleza mahitaji ya unyevu kwa mazao yaliyopo shambani. Mvua hizi ama huchelewa kuanza kunyesha na kusababisha kuchelewa kupanda mazao mashambani na kusababisha mazao kutokomaa vizuri, au zinanyesha nyingi na kuathiri maandalizi ya mashamba, upandaji na mazao yaliyopo shambani.
Yafuatayo ni majedwali yanayoonesha hali halisi ya uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu 2016/2017 pamoja na Utekelezaji na matarajio ya mavuno msimu wa mwaka 2017/18 hadi Jan. 2018:-
Jedwali No.3. Utekelezaji wa Malengo Msimu 2016/17
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA KILIMO MSIMU 2016/17 |
||||
Zao
|
Malengo kwa mwaka
|
Utekelezaji
|
||
Mazao ya Chakula
|
Eneo litakalopandwa (ha)
|
Matarajio ya mavuno (tani)
|
Eneo liliopandwa (ha)
|
Mavuno Halisi (tani)
|
Mahindi
|
38,202 |
95,505 |
27,885 |
69,713 |
Mpunga
|
108,865 |
381,027 |
101,056 |
353,696 |
Mtama
|
629 |
629 |
248.6 |
284.9 |
Uwele
|
0 |
0 |
0 |
0 |
Ulezi
|
7 |
4.2 |
6 |
6 |
Mihogo
|
9,572 |
191,440 |
1780 |
35600 |
Viazi vitamu
|
5,873 |
70,470 |
2041.6 |
24417.2 |
Ndizi mbivu
|
2,630 |
78,912 |
840.2 |
24346 |
Ndizi mbichi
|
4,678 |
131,880 |
2168 |
64130 |
Kunde
|
1,657 |
1,326 |
415 |
319.9 |
Maharage
|
217 |
195 |
152 |
150.8 |
Jumla Ndogo
|
172,330 |
951,388 |
136,592 |
572,664 |
|
|
|
|
|
Mazao ya Biashara
|
|
|
|
|
Miwa
|
5,909 |
472,744 |
5444.7 |
277420 |
Alizeti
|
912 |
1,368 |
24.8 |
37.3 |
Ufuta
|
10,145 |
10,145 |
3093.9 |
3145.5 |
Kakao
|
3,112 |
3,112 |
1462 |
1462 |
Nazi
|
1,919 |
13,435 |
1215.3 |
8555.1 |
Jumla Ndogo
|
21,997 |
500,804 |
11,241 |
290,620 |
|
|
|
|
|
Mazao Mengine
|
|
|
|
|
Embe
|
1,457 |
21,851 |
984 |
12,735 |
Chungwa
|
617 |
9,260 |
275.9 |
3,602 |
Tikiti maji
|
1,339 |
26,780 |
280.4 |
6,617 |
Vitunguu
|
391 |
7,814 |
10.4 |
183 |
Bamia
|
796 |
7,964 |
125.9 |
1,240 |
Nyanya
|
1,875 |
16,405 |
186.5 |
1,637 |
Nyanya chungu
|
1,199 |
8,994 |
237 |
1,807 |
Chinees Cabbage
|
847 |
10,585 |
142.7 |
1,812 |
Jumla Ndogo
|
8,521 |
109,653 |
2,242 |
29,632 |
Jumla Kuu
|
202,848 |
1,561,845 |
150,076 |
892,915 |
Jedwali No.5. Malengo ya Msimu 2017/18
MALENGO YA KILIMO NA UTEKELEZAJI MSIMU 2017/18 |
||||
Zao
|
Malengo kwa mwaka
|
Utekelezaji hadi Jan.2018
|
||
Mazao ya Chakula
|
Eneo litakalopandwa (ha)
|
Matarajio ya mavuno (tani)
|
Eneo liliopandwa (ha)
|
Mavuno Halisi (tani)
|
Mahindi
|
28,775 |
76,793 |
14,807.2 |
|
Mpunga
|
104,078 |
371,689 |
63,945.8 |
|
Mtama
|
1275.4 |
2353.3 |
33 |
|
Uwele
|
2 |
3 |
0 |
|
Ulezi
|
15 |
20.5 |
9.5 |
|
Mihogo
|
6,298 |
125,954 |
585.1 |
|
Viazi vitamu
|
4,719 |
56,599 |
760.4 |
|
Ndizi mbivu
|
2,436 |
71,464 |
1,837.2 |
|
Ndizi mbichi
|
5,306 |
156,883 |
4,196 |
|
Kunde
|
2,251 |
1,700 |
288.8 |
|
Maharage
|
228 |
280.8 |
122 |
|
Jumla Ndogo
|
155,383 |
863,740 |
86,585 |
0 |
|
|
|
|
|
Mazao ya Biashara
|
|
|
|
|
Miwa
|
4,029 |
201,450 |
3,461.1
|
|
Alizeti
|
1071.6 |
1,576 |
8.5
|
|
Ufuta
|
5,726 |
5,726 |
796
|
|
Kakao
|
4,691 |
4,668 |
595.7
|
|
Nazi
|
904 |
6,338 |
563.6
|
|
Jumla Ndogo
|
16,421 |
219,758 |
5,424.9
|
0 |
|
|
|
|
|
Mazao Mengine
|
|
|
|
|
Embe
|
1,083 |
16,181 |
960.5
|
|
Chungwa
|
312.6 |
4,699 |
211.2
|
|
Tikiti maji
|
488 |
9,246 |
161.1
|
|
Vitunguu
|
86.1 |
1,722 |
16.5
|
|
Bamia
|
290.9 |
2,909 |
160.4
|
|
Nyanya
|
456 |
4,009 |
144.8
|
|
Nyanya chungu
|
491 |
3,681 |
233.5
|
|
Chinese Cabbage
|
446.9 |
5,586 |
139.7
|
|
Jumla Ndogo
|
3,654 |
48,033 |
2,011.2
|
0 |
Jumla Kuu
|
175,458 |
1,131,530 |
94,021.1
|
0 |
3.0. Changamoto za Uzalishaji wa Mazao.
3.1. Udhibiti wa Visumbufu vya Mazao
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa