TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kama ifuatavyo;-
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 5.
SIFA ZA MWOMBAJI:-
Awe na Elimu ya Kidato cha Nne/ Sita
Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo.
Utawala
Rasilimali watu
Sheria
Maendeleo ya Jamii
Elimu ya Jamii
Usimamizi wa fedha au
Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali
Awe na Umri usiopungua miaka kumi na nane (18) na usiozidi Miaka arobaini na tano (45)
Awe amesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwenye kadi au namba ya usajili wa NIDA
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Viwango vya Serikali kwa ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi
MAJUKUMU YA KAZI
Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya Kijiji
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
MASHARTI YA JUMLA
Awe Raia wa Tanzania
“Testimonials Provisional Results, Statement of Result” na hati za matokeo kidato cha Nne na Sita (Form IV na VI na Result Slips) HAVITAKUBALIWA
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE NA TCU)
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI;-
Kila muombaji wa kazi awasilishe barua ikiambatishwa na;-
Wasifu Binafsi (CV)
Vivuli vya Vyeti Elimu na Ujuzi
Cheti cha Kuzaliwa
Picha mbili za “Passport Size”
Maombi yote yatumwe kupitia anuani ya posta kama ifuatavyo;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 263,
IFAKARA
1.7 Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 26/07/2021 siku ya Jumatatu ,saa 9.30 alasiri.
Tangazo hili limetolewa na Mhandisi Stephano Kaliwa, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa