Mashindano ya michezo kwa shule za msingi kwa mkoa wa Morogoro, yamezinduliwa jana huko Kilosa ambapo Halmashauri ya wilaya ya Mlimba imeshiriki kikamilifu kwenye michezo hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo ambao pia umeshuhudiwa na Mkurugezi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Eng. Stephano Kaliwa, Afisa elimu Msingi Bi Witness Kimoleta amesema kuwa timu zote zimejiandaa vya kutosha zipo tayari kushiriki kwenye michezo yote ambayo watapangiwa mbali na ile ambayo tayari imekwishachezwa, ambapo amesema kuwa ingawa kuna baadhi ya michezo wamepoteza ushindi lakini hawatokata tamaa, watajipanga upya na kufikia kwenye malengo waliyojiwekea.
Nae afisa vijana ambae pia ndio kocha wa michezo hiyo bwana Nicholaus Makata amesema kuwa mpaka sasa wamekwishacheza michezo mitano ambayo ni Mpira wa miguu wavulana na wasichana, mpira wa mikono, Netball, Mpira wa wavu, Pamoja na Riadha ambapo mpaka sasa wamepoteza michezo mitatu tu huku wakishika nafasi ya kwanza kwenye Riadha Pamoja na mpira wa miguu upande wa wanaume wameifunga malinyi mabao matatu kwa mawili huku wasichana wakitoka suluhu ya bila kufungana na Malinyi.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa katika mazungumzo yake na wanafunzi wa Halmashauri yake, amesema kuwa, michezo ni muhimu sana kwa kuimarisha afya ya masomo hivyo amewataka wanafunzi kuhakikisha kuwa Pamoja na masomo yao lakini pia wanatilia mkazo suala zima la michezo ili kuweza kufanikiwa katika vyote, aliongeza kuwa Halmashauri imeweza kuwasaidia kutoa kila wanachokihitaji ilimradi tu wahakikishe kuwa wanarudi nyumbani na ushindi ili iwe Fahari kwao na kwa Halmashauri yao kwa ujumla.
‘’Unajua vijana wangu michezo ni muhimu sana kwa kuimarisha Afya ya masomo yenu, hivyo ninawasihi mhakikishe kuwa mnatilia mkazo sana masomo yenu bila kusahau michezo ili muweze kufanikiwa katika vyote hivyo, Halmashauri yetu imeweza kutoa kila mtakachohitaji katika michezo hii, ilimradi tu muweze kufanya vizuri na kurudi na ushindi nyumbani, ili iwe Fahari kwenu na kwa Halmashauri kwa ujumla’’. Alimaliza Mhandisi Kaliwa
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa