Kaimu afisa elimu taaluma wa Mkoa wa Morogoro Mpangala amewataka wachezaji katika michezo ya UMITASHUNTA inayoendelea kujituma kwa bidii katika michezo hiyo kwa lengo la kupatikana kwa timu nzuri ya kufanya mashindano huko Mtwara.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa michezo hiyo (UMITASHUNTA) uliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Ifakara ambapo kauli mbiu katika michezo hiyo kwa mwaka 2019 ni Michezo na Sanaa kwa elimu bora na ajira.
Pia kaimu afisa elimu taaluma huyo amewaambia wanafunzi hao wawe watu wa kupenda michezo kwani michezo inajenga nguvu na afya katika miili yao na kuitaja michezo inayoshindaniwa ninpamoja na mpira wa mguu, mpira wa mikono, mpira wa pete, mpira wa wavu, mpira wa kengere, riadha pamoja na fani za ndani nyimbo na ngoma.
Aidha kwa upande wake Afisa michezo Mkoa wa MorogoroGrace Njau amesema kuwa hali ni shwari katika michezo, hakuna mgonjwa watoto wote ni wazima kutokana na kwamba hadi sasa hakuna majeruhi katika michezo hiyo .
Lakin I pia Njau amesema kuwa watotot wanatunzwas vizuri kama inavyopaswa nah ii ni kutokana na kupatiwa chakula ambacho kimechangwa na halmashauri kulingana na idadi ya wanafunzi walionao.
Hatahivyo ameeleza changamoto zinazoikabili michezo hiyo (UMITASHUNTA) ni pamoja na michango kwa baadhi ya Halmashauri hazijafikisha hata nusu ya kiwango kilichotakiwa kutolewa hivyo kupelekea ugumu kama wataendelea hivyo watafanyaje kwa huko baadae.
Sanjari na hayo amemuomba mgeni rasmi ndugu Mpangala azisisitize baadhi ya halmashauri ambazo hazijakamilisha michango, waweze kukamilisha na kwa wasiotoa kabisa waweze kutoa ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa